Pata taarifa kuu

Rekodi ya kishtoria ya mwanariadha wa Kenya Kelvin Kiptum yaidhinishwa

Nairobi – Shirikisho la riadhaa duniani limeidhinisha rekodi ya kihistoria ya dunia iliyowekwa na mwanariadha wa mbio za masafa marefu raia wa Kenya Kelvin Kiptum.

Kiptum aliweka rekodi mpya ya kuwa mwanariadha mwenye kasi zaidi katika historia ya mbio za masafa marefu
Kiptum aliweka rekodi mpya ya kuwa mwanariadha mwenye kasi zaidi katika historia ya mbio za masafa marefu AFP - KAMIL KRZACZYNSKI
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Oktoba mwaka uliopita, Kiptum aliweka rekodi mpya ya kuwa mwanariadha mwenye kasi zaidi katika historia ya mbio za masafa marefu.

Alimaliza mbio za Chicago Marathon kwa muda wa saa mbili na sekunde 35, sekunde 34 kutoka kwa rekodi ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na mwanariadha mahiri Eliud Kipchoge.

Kelvin Kiptum mwanariadha raia wa Kenya
Kelvin Kiptum mwanariadha raia wa Kenya REUTERS - ANDREW BOYERS

Kuidhinishwa kwa rekodi ya Kiptum na shirikisho la riadha za dunia kunamaanisha kuwa bodi inayosimamia riadha sasa inatambua kuwa inatambua rekodi yake  kwa mujibu washeria na kanuni za michezo.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 24 analenga kuweka historia tena mwezi Aprili kwa kuwa mtu wa kwanza kukimbia mbio za masafa marefu chini ya saa mbili, atakaposhiriki mbio za Rotterdam Marathon nchini Uholanzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.