Pata taarifa kuu

AFCON 2024: DRC kumenyana na Guinea katika robo-fainali

Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetinga robo fainali ya kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2023) kufuatia ushindi wa penalti 8-7 dhidi ya Mafarao katika dimba la Laurent Pokou, San Pedro.

Mchezaji wa Misri Zizo, katikati, akikabiliana na mchezaji wa DRC, Gedeon Kalulu, kushoto, wakati wa mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Misri na DR Congo kwenye Uwanja wa Laurent Pokou mjini San Pedro, Côte d'Ivoire, Jumapili Januari 28, 2024.
Mchezaji wa Misri Zizo, katikati, akikabiliana na mchezaji wa DRC, Gedeon Kalulu, kushoto, wakati wa mechi ya hatua ya 16 bora ya Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Misri na DR Congo kwenye Uwanja wa Laurent Pokou mjini San Pedro, Côte d'Ivoire, Jumapili Januari 28, 2024. AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

 

Wakongo hao walikomboa tikiti yao, na kuwatoa Wamisri kufuatia mikwaju mikali ya penalti, baada ya sare ya bao moja kwa moja kwenye mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Laurent Pokou huko San Pedro (Côte d’Ivoire).

Kikosi cha kocha Sébastien Désarbre kilifunga penalti nane dhidi ya saba za Wamisri, baada ya sare ya bao moja kwa moja kwenye mechi hiyo iliyokuwa na kazi ngumu.

Timu ya taifa ya DRC imefunga bao lake la kwanza katikadakika ya 37 ya mchezo kupitia mchezaji Yoane Wissa.

Na, Wamisri walisawazisha katika dakika ya 46 ya mchezo kupitia Moustapha Mohamed kwa mkwaju wa penalti.

Matokeo haya ylisalia bila kubadilika hadi kipenga cha mwisho kutoka kwa mwamuzi wa Afrika Kusini Souru Phatsoane.

DRC inafikia hatua hii, baada ya miaka 7 ilipopoteza kwa Ghana kwa bao 1 kwa 2.

Mechi ya DRC-Misri ilikuwa mpambano wa 5 kati ya mataifa haya mawili katika awamu ya mwisho ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mjini Kinshasa, wapenzi wengi wa soka wanataka kuona timu yao ikikurejea uzoefu wa mwaka 1974, wakati DRC, wakati huo ikiitwa Zaire, ilipoifunga Misri katika nusu fainali kabla ya kushinda kombe hili dhidi ya Zambia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.