Pata taarifa kuu

Aryna Sabalenka ashinda taji la pili la Australian Open

Nairobi – Na Paul Nzioki

Raia wa Belarus Aryna Sabalenka amemshinda Mchina Zheng Qinwen na kuhifadhi taji la Grand slam kwa wanawake katika michuano ya Tenisi Australia Open.
Raia wa Belarus Aryna Sabalenka amemshinda Mchina Zheng Qinwen na kuhifadhi taji la Grand slam kwa wanawake katika michuano ya Tenisi Australia Open. REUTERS - EDGAR SU
Matangazo ya kibiashara

Bingwa mtetezi wa michuano ya Tenisi Australia open kwa upande wa Kinadada, ameshinda taji hilo na kupata ushindi wake wa pili wa Grand Slam.

Raia wa Belarus Aryna Sabalenka amemshinda Mchina Zheng Qinwen na kuhifadhi taji la Grand slam kwa wanawake katika michuano ya Tenisi Australia Open.

Sabalenka amepata alama 6-3 katika seti ya kwanza na alama 6-2 katika seti ya pili katika mchezo huo wa fainali akishinda bila kuachia seti moja.

Mashindano ya mchezo wa Tenis ya Australian Open
Mashindano ya mchezo wa Tenis ya Australian Open REUTERS - EDGAR SU

Sabalenka anaorodheshwa katika nafasi ya pili duniani huku mpinzani wake katika fainali hio Zheng akiorodheshwa katika nafasi ya 12.

Sabalenka ni mwanamke wa kwanza kushinda mfululizo katika fainali tangu Victoria Azarenka mwaka 2013.

Baada ya Iga swiatek kushindwa katika raundi ya tatu, Sabalenka mwenye umri wa miaka 25, alikua kipenzi kikubwa cha mashindnao na akaiga mwenzake Azarenka kwa ushindi ambao ulichukua zaidi ya saa moja.

"Imekuwa wiki kadhaa za kushangaza na sikuweza kufikiria kunyanyua kombe wakati mwingine," Sabalenka alisema.

Zheng, mwenye umri wa miaka 21, alikuwa akicheza fainali yake kuu ya kwanza na mara nyingi alionekana kushtushwa na hafla hiyo na mpinzani wake.

Aryna Sabalenka amemshinda Zheng Qinwen raia wa China
Aryna Sabalenka amemshinda Zheng Qinwen raia wa China REUTERS - EDGAR SU

Zheng hajafanikisha ndoto za mashabiki wake

Zheng ameshindwa kufikia matarajio ya mashabiki wake kutoka nchini China waliofika uwanjani kumshabikia dhidi ya Sabalenka.

Mashabiki wengi walimtaka mchezaji huyo kuiga mfano wa Li na Azarenka.

Nyota wa nchini China Li alishinda mashindano ya Australian Open 2014 kwa furaha ya taifa, kitu kilichomfanya Zheng aliyekua na umri wa miaka 11 kupenda sana mchezo wa Tenisi.

Qinwen Zheng(kulia) akiwa na raia wa Belarus Aryna Sabalenka
Qinwen Zheng(kulia) akiwa na raia wa Belarus Aryna Sabalenka REUTERS - EDGAR SU

Pamoja na kuonekana mwenye jazba, Zheng hakuweza kustahimili kasi ya Sabalenka .

"Ni fainali yangu ya kwanza na ninasikitika kidogo lakini limekua zoezi nzuri la kupata uzoefu," alisema Zheng, ambaye ataingia kwenye 10 bora duniani kwa mara ya kwanza wakati viwango vitachapishwa. Jumatatu.

"Ninahisi ningefanya vyema zaidi lakini sikufanya hivyo kwenye mechi hii." Zheng aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.