Pata taarifa kuu

AFCON: Nigeria yatamba mbele ya Cote Dvoire

Nairobi – Penalti ya nahodha William Troost-Ekong' katika kipindi cha pili iliisaidia Nigeria kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cote Dvoire katika mechi ya pili, kuwania kombe la mataifa ya Afrika AFCON. 

Nigeria imepata ushindi dhidi ya Ivory Coast
Nigeria imepata ushindi dhidi ya Ivory Coast AP - Sunday Alamba
Matangazo ya kibiashara

 

Matokeo haya yanaiweka Cote Dvoire kwenye nafasi ngumu ya kufuzu kwenye hatua ya 16 bora. 

Bao la Nigeria lilifungwa dakika 10 baada ya kipindi cha pili cha mchuano huo, kwenye uwanja wa Olimpiki wa Ebimpe jijini Abidjan, baada ya kuchezewa ndivyo sivyo kwa mshambuliaji wa Super Eagles Victor Osimhen. 

Ushindi huu wa Nigeria unakuja baada ya kulazimishwa sare ya bao 1 kwa 1 na Equatorial Guinea kwenye mechi yake ya ufunguzi. 

Shabiki wa Ivory Coast wakati wa mechi kati ya timu yake dhidi ya Nigeria
Shabiki wa Ivory Coast wakati wa mechi kati ya timu yake dhidi ya Nigeria REUTERS - STRINGER

Kocha wa Nigeria, Jose Peseiro, amesema ushindi wa timu yake imeleta matumaini makubwa licha ya kukiri kuwa wenyeji pia wana timu zuri. 

“Timu yetu ilikuwa nzuri ndio sababu tukapata ushindi, lakini wapinzani wetu wana kikosi kizuri,” amesema. 

Nigeria na Equatorial Guinea kila mmoja ana alama nne katika kundi A. Equatorial Guinea walipata ushindi mkubwa baada ya kuilaza Guinea-Bissau 4-2 katika mechi yake ya pili. 

Licha ya kuwa timu tatu bora kufuzu katika hatua ya mwondoano, ni lazima Cote Dvoire iishinde Equatorial Guinea ili kufuzukatika hatua hiyo

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.