Pata taarifa kuu

AFCON 2024: Nigeria watoka sare na Equatorial Guinea ya kufungana 1-1

Nigeria, ambao walitawala mpira, walibana na Equatorial Guinea na hivyo kutoka sare ya 1-1 Jumapili kwa kucheza kwa kundi A kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika huko Abidjan.

Mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen akitazama mechi ya Kundi A ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)  2024 kati ya Nigeria na Equatorial Guinea kwenye uwanja wa Alassane Ouattara huko Ebimpe, Abidjan, Januari 14, 2024.
Mshambuliaji wa Nigeria, Victor Osimhen akitazama mechi ya Kundi A ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2024 kati ya Nigeria na Equatorial Guinea kwenye uwanja wa Alassane Ouattara huko Ebimpe, Abidjan, Januari 14, 2024. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Nigeria, mshindi mara tatu wa AFCON (1980, 1994, 2013), hawakuchukua fursa ya uwiano mzuri wa nguvu na kujikuta wakiwa na pointi mbili nyuma ya Côte d'Ivoire, iliyoshinda siku moja kabla dhidi ya Guinea Bissau (2-0) katika mechi ya ufunguzi wa toleo hili la 34.

Bao la Equatorial Guinea lilipachikwa wavuni na Ivan Salvadorkatika dakika ya 36 ya mchezo. Na bao la kusawazisha la Nigeria lilifungwa Victor Osimhen katika dakika ya 38 ya mchezo.

Muda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza kwenda mapumziko, Moses Simon alikaribia sana kuipa Nigeria bao la pili, lakini shuti lake lilirudishwa na kipa wa Equatorial Guinea Jesus Owono (45 + 3). 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.