Pata taarifa kuu

Wachezaji 10 wakuangaziwa kwenye kipute cha AFCON 2023

Nairobi – Katika muda wa siku chache zijazo, bara Afrika litakuwa litakuwa likiandaa awau ya 34 ya mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika ambayo yatafanyika nchini Côte d'Ivoire.

Mohamed Salah wa Misri na Vincent Aboubakar wa Cameroon.
Mohamed Salah wa Misri na Vincent Aboubakar wa Cameroon. © Charly Triballeau/AFP/Kenzo Tribouillard
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya wachezaji wa tajiriba wanatarajiwa kuonyesha ubora wao kwenye kipute hicho kati ya tarehe 13 ya mwezi Januari hadi Februari 11.

Miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na:

Sadio Mané (Senegal, 31)

Sadio Mané kwa sasa anacheza katika ligi ya Saudi Arabia
Sadio Mané kwa sasa anacheza katika ligi ya Saudi Arabia © Pierre René-Worms

Aliteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya awamu iliyopita, mchezaji muhimu katika kikosi cha Simba wa Teranga, anatarajiwa kuwa mwenye mchango mkubwa haswa wakati pia akipewa majukumu ya kuwa nahodha wa timu yake ya taifa kutetea ubingwa wa mashindano haya.

Baada ya kuhamia Saudi Arabia akitokea barani Ulaya katika msimu uliopita, Sadio Mané hajapoteza makali yake.

Vincent Aboubakar (Cameroon, 31)

Vincent Aboubakar, anaelekea Ivory Coast akiwa na jukumu la kupachika magoli
Vincent Aboubakar, anaelekea Ivory Coast akiwa na jukumu la kupachika magoli © Pierre René-Worms

Katika mashindano kadhaa, amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Indomitable Lions. Vincent Aboubakar ni nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon ambaye pia amepewa majukumu ya kuisaidia nchi yake kupata magoli.

Tajiriba yake na uongozi ikitarajiwa kuongezea kikosi cha Cameroon nguvu.

Sehrou Guirassy (Guinea, 27)

Kiungo huyo wa kati ameonekana kuaanza kuimarika huko Ujerumani ambapo amekuwa akiwapa washambuliaji wenginge katika ligi ya Bundesliga upinzani.

Sébastien Haller (Côte d'Ivoire, 30)

Sébastien Haller, anatazamiwa kutumia ubora wake kuisaidia timu yake kupiga hatua
Sébastien Haller, anatazamiwa kutumia ubora wake kuisaidia timu yake kupiga hatua © Pierre RENÉ-WORMS/RFI

Anashiriki mashindano haya kwa mara ya pili ambapo kwa sasa anacheza katika ardhi ya nyumbani mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.

Akiwa na umri wa miaka 29, Sébastien Haller, anatazamiwa kutumia ubora wake kuisaidia timu yake kupiga hatua.

Mohamed Amoura (Algeria, 23)

Kiungo huyo wa kati amekuwa akifanya vyema katika klabu yake ya huko nchini Ubelgiji na ana uwezo wa kuogoza nchi yake katika mashindano makubwa kama haya ya AFCON.

Victor Osimhen (Nigeria, 25)

Victor Osimhen, Mchezaji bora barani Afrika 2023
Victor Osimhen, Mchezaji bora barani Afrika 2023 © rfi fulfulde

Anashiriki AFCON ya mwaka huu akiwa mchezaji bora wa mwaka barani Afrika ambapo tajiriba yake katika ligi ya Ulaya inampa nafasi bora ya kuwaongoza wachezaji wenzake katika kipute cha mwaka huu.

Azzedine Ounahi (Morocco, 24)

Alikuwa kwenye kikosi cha Morocco wakati wa kombe la dunia la mwaka wa 2022 na kwa sasa pia ana nafasi ya kuonyesha viwango vyake katika mechi hizi.

Mohammed Kudus (Ghana, 23)

Mohammed Kudus amekuwa akifanya vyema akiwa na klabu yake ya West Ham
Mohammed Kudus amekuwa akifanya vyema akiwa na klabu yake ya West Ham REUTERS - KAI PFAFFENBACH

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amekuwa na mchezo bora katika klabu yake ya West Ham inayoshiriki katika ligi kuu ya Uingereza.

Mohamed Salah (Egypt, 31)

Fainali hii ni ya tatu kwa Mohamed Salah kushiriki
Fainali hii ni ya tatu kwa Mohamed Salah kushiriki © Pierre René-Worms

Kama alivyofanya kwenye fainali tatu zilizopita, Mohamed Salah kwa mara nyengine tena kubeba nchi yake na kuisaidia kushinda taji hili.

Salah amekuwa nyota ya kalbu ya Liverpool, akiisaidia klabu hiyo katika ufungaji wa mabao.

Peter Shalulile (Namibia, 30)

Peter Shalulile, yuko katika ubora wake katika klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.