Pata taarifa kuu

Kandanda: Kocha wa timu ya taifa ya Brazil Fernando Diniz atimuliwa

Kocha wa timu ya taifa ya Brazil, Fernando Diniz, ametimuliwa kwenye timu hiyo tangu siku ya Ijumaa, chanzo ndani ya Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) kimeliambia shirika la habri la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.

Fernando Diniz, kocha wa timu ya Brazil, katika mkutano na waandishi wa habari, huko Lima (Peru), Septemba 11, 2023.
Fernando Diniz, kocha wa timu ya Brazil, katika mkutano na waandishi wa habari, huko Lima (Peru), Septemba 11, 2023. © Martin Mejia/AP
Matangazo ya kibiashara

Diniz aliteuliwa mwezi wa Julai 2023, lakini matokeo mabaya ya Selecao yalimgharimu nafasi yake.

Brazil imeshinda mechi mbili pekee kati ya sita ilizocheza tangu kuanza kwa mechi za timu za Amerika Kusini zilizotinga kwa michuno ya Kombe la Dunia la 2026, ambalo litapigwa nchini Maekani, Canada na Mexico.

Mwaka mmoja baada ya kuondolewa katika robo-fainali ya Kombe la Dunia la mwaka 2022 nchini Qatar na Croatia, "Canarinha" wako katika nafasi ya sita kati ya kumi katika viwango vya kufuzu, ikiwa na pointi mbili pekee mbele ya nafasi ya mchujo. Inatia wasiwasi kutofanya vizuri kwa taifa pekee lililoshiriki katika matoleo 22 ya Kombe la Dunia, na mataji matano, ikiwa ni rekodi.

Baada ya kuondoka kwa Tite (2016-2022), matarajio makubwa yalimzunguka Diniz.

Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 49 aliteuliwa kwa mwaka mmoja, wakati akiwa mkufunzi wa klabu ya Rio Fluminense, ambayo ilishinda Copa Libertadores mwishoni mwa mwaka 2023.

Mamlaka yake yalionekana kama kipindi cha muda akimsubiri Carlo Ancelotti, ambaye kuwasili kwake kulisubiriwa kwa hamu hata kama kocha huyo wa Italia alikuwa mwangalifu kutothibitisha hilo. "Il mister" aliishia kukataa, na kuongeza mkataba wake na Real Madrid mwishoni mwa mwezi wa Desemba hadi mwezi wa Juni 2026.

Kufukuzwa kwa Diniz kunakuja siku moja baada ya mabadiliko katika mzozo mwingine, huu wa kitaasisi, ambao unatikisa soka ya Brazil: rais wa CBF Ednaldo Rodrigues, aliyefukuzwa mwanzoni mwa mwezi wa Desemba na mahakama huko Rio, alirejeshwa kwenye nafasi yake kwa uamuzi wa jaji wa Mahakama ya Juu.

Uamuzi wa mahakama ya Carioca ulikuwa umebatilisha makubaliano ya awali kati ya CBF na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Rio, ya kuanzia mwezi Machi 2022, ambayo yaliwezesha kuchaguliwa kwa rais wa kwanza mweusi wa shirikisho hilo.

Lakini FIFA na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (Conmebol) hawakuona uamuzi huu wa mahakama ipasavyo, wakikataa kuingiliwa kwa serikali katika masuala ya CBF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.