Pata taarifa kuu

Morocco yaungana na Uhispania na Ureno kwa zabuni ya pamoja ya Kombe la Dunia la 2023

Mashirikisho ya soka ya Ulaya, Afrika na Amerika Kusini yamekubaliana juu ya mgombea mmoja wa Kombe la Dunia la 2030, lililowasilishwa na Morocco, Uhispania na Ureno pamoja na mechi tatu Amerika Kusini, FIFA imetangaza Jumatano.

Baada ya AFCON 2025, Morocco inaweza kupata - kwa pamoja na Uhispania na Ureno - idhini ya kuanda michuano ya Kombe la Dunia la 2030.
Baada ya AFCON 2025, Morocco inaweza kupata - kwa pamoja na Uhispania na Ureno - idhini ya kuanda michuano ya Kombe la Dunia la 2030. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa miaka 100 ya toleo lake la kwanza nchini Uruguay, Kombe la Dunia la Wanaume "litaunganisha mabara matatu na nchi sita", limeahidi shirika la mpira wa miguu, ambalo litaidhinisha vigezo vya kiufundi na halitatoa tuzo rasmi hadi mwisho wa mwaka 2024.

Lakini kwa idhini ya " kauli moja" ya faili hii ya kipekee iliyotolewa na Baraza la FIFA, njia inaonekana wazi kwa muundo huu wa kimataifa usio na kifani, kuahidi usanidi tata wa kisiasa na wa vifaa na maswali mengi juu ya athari ya mazingira ya hafla kuu za michezo.

Tangazo la Jumatano linahitimisha uhasama uliotangazwa kati ya nchi mbili zilizopendekezwa, barua ya pamoja ya kuwania kutoka Argentina, Uruguay, Chile na Paraguay, na tikiti ya Ulaya inayoongozwa kwa muda mrefu na Uhispania na Ureno.

Mwaka mmoja uliopita, kwa uungwaji mkono wa UEFA, nchi hizo mbili ziliijumuisha Ukraine katika faili yao, na kuhakikisha wanataka kuzindua "ujumbe wa mshikamano na matumaini" nakutoa heshima kwa "ustahimilivu na ujasiri" wa nchi inayokaliwa na jeshi la Urusi. tangu mwezi Februari 2022.

Makubaliano kati ya UEFA na washirika wake wa Afrika (CAF) na Amerika Kusini (CONMEBOL) yanaidhinisha kujiondoa kwa Ukraine na kuondolewa kwa mradi wa awali wa Argentina-Chile-Uruguay-Paraguay, badala ya ishara kuu ya makubaliano.

Kulingana na Fifa, "sherehe ya miaka mia moja" itafanyika "kwenye uwanja ambapo yote yalianza", huko Montevideo, wakati hafla hiyo ilileta pamoja timu 13 katika jiji moja mwenyeji - ikilinganishwa na timu 32 wakati wa Kombe la Dunia la mwaka 2022 nchini Qatar na nchi 48 kuanzia toleo la mwaka 2026 nchini Marekani, Canada na Mexico. Hata hivyo, Montevideo, Asuncion na Buenos Aires kila moja itakuwa mwenyeji wa mechi ya Kombe la Dunia, hata ikiwa hafla nyingi zitafanyika kati ya nchi tatu zinazoandaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.