Pata taarifa kuu

Harry Kane amejiunga na Bayern Munich

Nairobi – Nahodha wa Uingereza Harry Kane amejiunga na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kwa mkataba wa miaka minne na hivyo kuhitimisha maisha yake ya soka yaliyovunja rekodi katika klabu ya Tottenham.

Mchezaji huyo raia wa Uingereza, amejiunga na klabu ya Bayern Munich
Mchezaji huyo raia wa Uingereza, amejiunga na klabu ya Bayern Munich © Bayern Munich
Matangazo ya kibiashara

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wenye thamani ya zaidi ya euro 110m na anaweza kucheza mechi yake ya kwanza katika mchezo wa Jumamosi wa kombe la Super Cup dhidi ya RB Leipzig.

Kane, 30, anaondoka kwenye klabu ya Spurs ya ligi kuu ya Uingereza kama mfungaji bora wa muda wote akiwa na mabao 280 katika mechi 435.

Katika chapisho lake kwenye mtandao wa kijamii alisema "alihisi huu ulikuwa wakati wa kuondoka" Spurs.

Mustakabali wa Kane ulikuwa haujulikani majira yote ya kiangazi kwa sababu alikuwa amesalia na  mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake na Spurs.

Ameshinda kiatu cha dhahabu kwenye ligi kuu ya Uingereza mara tatu - 2015-16, 2016-17 na 2020-21 - na akiwa na mabao 213 kutoka kwa mechi 320 kwenye ligi kuu ya Uingereza, alihitaji tu 48 zaidi ili kuvunja rekodi ya ufungaji ya Alan Shearer ya ligi kuu.

Kane, ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote wa Uingereza akiwa na mabao 58 ya kimataifa, hajawahi kushinda kombe lolote akiwa na klabu au nchi.

Bayern Munich walitwaa taji lao la 33 la Bundesliga msimu uliopita na la 11 mfululizo na wameshinda ligi ya mabingwa mara sita na Kombe la Ujerumani mara 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.