Pata taarifa kuu

Australia imewaondoa Ufaransa kwenye kombe la dunia

Nairobi – Australia sasa itamenyana na washindi wa mchujo wa mwisho wa nane bora kati ya Uingereza na Colombia baada ya kuwashinda ufaransa katika mechi ya kuwania ubingwa wa dunia upande wa wanawake.

Australia sasa itamenyana na washindi wa mchujo wa mwisho wa nane bora kati ya Uingereza na Colombia
Australia sasa itamenyana na washindi wa mchujo wa mwisho wa nane bora kati ya Uingereza na Colombia AP - Tertius Pickard
Matangazo ya kibiashara

Baada ya sare ya 0-0 katika mda wa dakika 120,  mechi hiyo iliingia  katika hatua ya penalti, Cortnee Vine akifunga penalti ya ushindi baada ya timu zote kupiga mikwaju 10.

Vicki Becho alikosa penalti ya 10 ya Ufaransa, na ikasalia kwa Vine kuivusha Australia kwa kumshinda kipa wa akiba wa Ufaransa, Solene Durand. Pambano hilo lilitazamwa na umati wa watu 49,461.

Mwaka huu kutakuwa na bingwa mpya baada ya bingwa wa sasa Marekani kuondolewa
Mwaka huu kutakuwa na bingwa mpya baada ya bingwa wa sasa Marekani kuondolewa AP - Tertius Pickard

Les Bleues walikuwa na matumaini ya kufika nusu fainali kwa mara ya pili, kufuatia kushindwa katika mechi nne za mwisho mwaka 2011, lakini badala yake wamerudi nyumbani.

Kocha wa Australia, Matildas Tony Gustavsson alisalia na timu ile ile iliyoanza dhidi ya Denmark katika hatua ya 16 bora, huku Ufaransa ikimrejesha kwenye safu ya ulinzi Maelle Lakrar.

Tayari timu zote za bara Afrika zimeyaaga mashindano huku bara Ulaya likiwa limesalia na wawakilishi 3 ambapo tayari Sweden na Uhispania watakutana katika nusu fainali ya kwanza.

Les Bleues walikuwa na matumaini ya kufika nusu fainali kwa mara ya pili
Les Bleues walikuwa na matumaini ya kufika nusu fainali kwa mara ya pili AFP - FRANCK FIFE

Taifa lingine la bara Ulaya Uingereza wanakabiliana na Colombia katika mchezo wa robô fainali.

Bingwa mtetezi Marekani katika Makala mwaka 2019 yaliyoandaliwa nchini Ufaransa, ameondolewa katika mashindano ikiwa na maana sasa makala ya mwaka huu yatakuwa na bingwa mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.