Kombe la dunia: Marekani imetoka sare ya bao 1 kwa 1 na Uholanzi
Nairobi – Katika michuano ya kombe la dunia kwa wanawake katika mchezo wa soka, inayoendelea nchini New Zealand na Australia.
Imechapishwa:
Marekani imetoka sare ya bao 1 kwa 1 na Uholanzi, katika mechi ya kundi E iliyomilikiwa saa chache zilizopita.
Baadaye leo, katika mji wa Dunedin, nchini New Zealand, Ureno itachuana na Vietnam, katika mechi ya kundi E huku, Australia nayo itamenyana na Nigeria katika mechi ya kundi B.
Katika mechi ya kwanza, Nigeria haikufungana na Canada ambayo jana katika mechi yake ya pili, iliishinda Jamhuri ya Ireland mabao 2 kwa 1 .
Wawakilishi wengine wa Afrika, Zambia jana walicharazwa mabao 5 kwa 0 na Hispania katika mechi ya kundi C, mechi ya kwanza Zambia pia ilifungwa mabao 5 kwa 0 na Japan.
Afrika Kusini na Morocco pia ni wawakilishi wengine wa Afrika na hawajapata ushindi wowote mpaka sasa.