Pata taarifa kuu

Kombe la dunia: Nigeria yapata alama moja dhidi ya Canada

Nairobi – Na mwandishi wetu Paul Nzioki

Canada ilitoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Nigeria katika mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake
Canada ilitoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Nigeria katika mashindano ya kombe la dunia kwa wanawake AP - Hamish Blair
Matangazo ya kibiashara

Christine Sinclair alikosa nafasi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michuano sita ya kombe la dunia la Fifa kwa wanawake huku Nigeria ikipata sare dhidi ya Canada.

Kipa wa Nigeria, Chiamaka Nnadozie alizuia mkwaju wa penalti wa Sinclair mapema katika kipindi cha pili huku mabingwa hao wa Olimpiki wakichanganyikiwa kwa kukosa nafasi hiyo mjini Melbourne.

Canada na Nigeria sasa wapo nyuma ya wenyeji Australia katika kundi B.

Canada walipoteza penalti wakati wa mechi yao dhidi ya Nigeria
Canada walipoteza penalti wakati wa mechi yao dhidi ya Nigeria REUTERS - HANNAH MCKAY

Canada itachuana na Jamhuri ya Ireland katika mchezo unaofuata tarehe 26 Julai, baada ya Ireland nao kupoteza dhidi ya Australia siku ya Alhamisi.

Nahodha Sinclair aliingia mchezoni akilenga kutengeneza historia ya kibinafsi. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alikuwa akicheza mechi yake ya 324 kimataifa na ameifungia nchi yake mabao 190.

Nigeria, imeorodheshwa katika nafasi ya 33 chini ya Canada katika viwango vya Fifa.
Nigeria, imeorodheshwa katika nafasi ya 33 chini ya Canada katika viwango vya Fifa. REUTERS - HANNAH MCKAY

Yeye ni mmoja wa wachezaji watatu waliofunga kwenye fainali tano za kombe la dunia la Fifa kwa wanawake zilizopita - pamoja na Marta na Cristiano Ronaldo.

Mwamuzi Lina Lehtovaara alitoa penalti hiyo baada ya mwamuzi msaidizi wa video kuingilia kati, hata hivyo juhudi za Sinclair zilikuwa dhaifu baada ya mkwaju wake kuokolewa na kipa wa Nigeria Nnadozie.

"Pengine nitampa sifa nyingi, lakini nadhani ni mmoja wa makipa bora chipukizi duniani," alisema kocha wa Nigeria Randy Waldrum.

Nigeria, imeorodheshwa katika nafasi ya 33 chini ya Canada katika viwango vya Fifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.