Pata taarifa kuu

Tobi Amusan, atuhumiwa kwa kukiuka sheria za matumizi ya dawa zilizopigwa marafuku

Nairobi – Mwanariadha Tobi Amusan, raia wa Nigeria amesema ameshtakiwa kwa makosa ya kukiuka sheria za matumizi ya dawa zilizopigwa marafuku.

Tobi Amusan, mwanariadha wa Nigeria
Tobi Amusan, mwanariadha wa Nigeria © REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Amusan ni bingwa wa dunia katika mbio za mita 100 kuruka viunzi.

Kitengo cha maadili katika riadha kimemtuhumu mwanariadha huyo kwa kukosa kufanya vipimo vitatu katika kipindi cha miezi 12.

Mwanariadha huyo huenda akapigwa marufuku ya miaka mwili kushiriki katika mashindano ya riadha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Amusan mwenye umri wa miaka 26 amesema kwamba hana hatia.

Aidha ameeleza kuwa atahakikisha anamaliza changamoto inayomkabili iliaweze kushiriki katika mbio za dunia mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.