Pata taarifa kuu

Arsenal wamekamilisha usajili Declan Rice kutoka West Ham

Nairobi – Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Declan Rice amejiunga na Arsenal kutoka West Ham United kwa mkataba wa muda mrefu.

Declan Rice, Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza amejiunga na Arsenal kutoka West Ham
Declan Rice, Mchezaji wa timu ya taifa ya Uingereza amejiunga na Arsenal kutoka West Ham AFP
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 tayari ana uzoefu mkubwa, akicheza mechi 245 akiwa na The Hammers na pia kushinda mechi 43 akiwa na Three Lions.

Declan alianza taaluma yake ya soka katika klabu ya Chelsea, kabla ya kujiunga na akademi ya West Ham mwaka 2014, na alisaini mkataba wake wa kwanza wa kitaaluma mwaka mmoja baadaye.

Mchezaji huyo amejiunga na Arsenal kutoka West Ham
Mchezaji huyo amejiunga na Arsenal kutoka West Ham © Arsenal

Katika siku ya mwisho ya msimu wa 2016/17, Declan mwenye umri wa miaka 18 alicheza mechi yake ya kwanza na hivi karibuni akawa sehemu muhimu ya kikosi chao cha kwanza kwa misimu sita iliyofuata.

Alitangazwa kuwa nahodha wa klabu hiyo mnamo Mei 2022 ambapo pia alishiriki katika michuano ya Euro 2020 na Kombe la Dunia la FIFA la 2022 akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza.

Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Arsenal, Edu, alisema Declan ni mchezaji mwenye tajiriba ya juu  ambapo mchango wake utakuwa muhimu katika klabu hiyo ya Uingereza.

Meneja Mikel Arteta kwa upande wake ameeleza kuwa wamefurahia sana kwamba Declan anajiunga nao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.