Pata taarifa kuu

Carlo Ancelotti kuinoa Brazil kuanzia Juni 2024

Muitaliano Carlo Ancelotti atakuwa kocha wa Brazil kuanzia michuano ya Copa America 2024, iliyopangwa kuanza mwezi Juni na Julai mwaka ujao nchini Marekani, mara tu mkataba wake na Real Madrid utakapofikia kikomo, chanzo kutoka Shirika la Soka nchini Brazili (CBF) kimeliambia shirikala habari la AFP.

Muitaliano huyu hata hivyo alikuwa ametangaza mara kadhaa kwamba atastaafu baada ya kibarua hiki cha mwisho ndani ya Real, baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takriban miaka thelathini.
Muitaliano huyu hata hivyo alikuwa ametangaza mara kadhaa kwamba atastaafu baada ya kibarua hiki cha mwisho ndani ya Real, baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takriban miaka thelathini. POOL/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

CBF imesema katika taarifa kwamba mchezaji wa Fluminense mwenye makazi yake Rio de Janeiro Fernando Diniz ataongoza timu hiyo ambayo ni mabingwa mara tano wa dunia hadi Ancelotti atakapochukua nafasi ya meneja.

Meneja huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 64 yuko chini ya mkataba na Real Madrid hadi :mwezi Juni 2024 na amesema hadharani kwamba anataka kuendelea hadi wakati huo.

Tangazo hili, lililotolewa na chanzo cha ngazi ya juu ndani ya CBF ambacho hakikutaka kutajwa jina, kinahitimisha mazungumzo ya miezi kadhaa kati ya Ancelotti na mkuu wa shirikisho la Brazil, Ednaldo Rodrigues, ambaye amekuwa akimchukulia Ancellotti kama chaguo lake.

Kocha wa Brazil, Tite, ambaye amekuwa kwenye nafasi hiyo tangu 2016, aliacha wadhifa wake baada ya timu ya Brazil kushindwa dhidi ya Croatia katika robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar mwezi Disemba.

Ancelotti atakuwa mgeni wa nne kuchukua hatamu za Selecao, wa kwanza katika takriban miaka 60.

Muitaliano huyo hata hivyo alikuwa ametangaza mara kadhaa kwamba atastaafu baada ya kibarua hiki cha mwisho ndani ya Real, baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takriban miaka thelathini.

Lakini hatimaye alikubali kushawishiwa na Brazil, nchi ambayo soka ni mfalme, kuchukua udhibiti wa Selecao ambayo si ndoto tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.