Pata taarifa kuu

U23 AFCON : Morocco na Misri zatinga fainali na kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ya Paris

Morocco, nchi mwenyeji, na Misri, bingwa mtetezi, watacheza fainali ya AFCON kwa wachezaji walio na umri ulio chini ya miaka 23 baada ya ushindi wao mtawalia mbele ya Mali (2-2, tab 4-3) na Guinea (1-0). Timu zote mbili zilifuzu moja kwa moja kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris. Tikiti ya tatu kwa Afrika itachezwa kati ya timu zitakazoshindwa katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu.

Timu ya Morocco, imetinga fainali ya U23 AFCON, pia watakuwa Paris kwa Michezo ya Olimpiki ya 2024.
Timu ya Morocco, imetinga fainali ya U23 AFCON, pia watakuwa Paris kwa Michezo ya Olimpiki ya 2024. © Courtesy of CAF
Matangazo ya kibiashara

Mantiki hiyo iliheshimiwa katika nusu-fainali hizi za U23 AFCON  ambazo zilibishaniwa Jumanne hii, Julai 4. Lakini kazi ilikuwa ngumu zaidi kwa Morocco, nchi mwenyeji, ambayo hata hivyo ilikuwa imevuka raundi ya kwanza na ushindi mara tatu katika mechi tatu na mabao manane. Nusu fainali ilikuwa ngumu kusema kidogo kwa Atlas Cubs ambao walilazimika kusubiri muda wa ziada na mikwaju ya penalti kuwashinda Mali waliokuwa wamejizatiti vilivyo. Hata hivyo, Zakaria El Ouahdi alikuwa ameimarisha ubabe wa timu yake mwanzoni mwa mechi kwa kufungua bao katika robo ya kwanza ya saa (dakika 14). Hata hivyo bao la kusawaziha lilifungwa na Mamady Diambou katika dakika ya 66ya mchezo.

Olimpiki ya kumi na tatu kwa Misri

Wafuasi wengi wa Morocco waliokuwepo kwenye Uwanja wa Stade Moulay Abdallah waliamini kuwa mechi imemalizika baada ya bao la Amani El Ouazzani kipindi cha pili, baada ya kipindi cha ziada (108), lakini bila kutegemea uimara wa Mali ambao walikuwa na ndoto ya kucheza AFCON yao ya kwanza. Issoufi Maiga alisawazisha kwa mara ya pili kwa upande wa Mali na kuwalazimisha wenyeji kupiga mikwaju ya penalti.

Katika zoezi hili, Wamorocco wana ustadi zaidi, kufikia raundi ya wazi kwenye mikwaju yao minne ya kwanza. Kinyume chake, nahodha wa Mali Boucacar Traoré alikosa bao kabla ya Ahmed Diomandé kukosa bao lingine kupitia mikwaju ya penalti na hivyo kuipa Morocco kufuzu katika fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.