Pata taarifa kuu

Munyantwali achaguliwa rais mpya wa soka nchini Rwanda

Na: Jason Sagini

Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Rwanda Alphose Munyantwali
Rais mpya wa Shirikisho la soka nchini Rwanda Alphose Munyantwali © ferwafa
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa klabu ya Police FC inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Rwanda, Alphose Munyantwali amechaguliwa kuwa rais mpya wa shirikisho la soka nchini humo (FERWAFA) kwa miaka miwili ijayo.   

Munyantwali alipigiwa kura katika mkutano mkuu jijini Kigali Jumamosi iliyopita, katika uchaguzi ulioshuhudiwa   na mjumbe wa baraza la FIFA Amaju Pinnick kutoka Nigeria na mjumbe wa CAF ambaye pia ni rais wa shirikisho la soka nchini Uganda (FUFA) Moses Magogo. 

Wajumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la soka nchini Rwanda. 24/06/2023
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la soka nchini Rwanda. 24/06/2023 © ferwafa

Uchaguzi huu ulifanyika miezi miwili baada ya Olivier Mugabo Nizeyimana kujiuzulu kwa sababu za kibinfasi. Munyantwali alichaguliwa bila ya kuwa na mpinzani akijizolea jumla ya kura 50 kati ya 56 za wajumbe wa kongamano hilo.  

Katika nafasi nyingine kwenye baraza la FERWAFA, Marcel Matiku Habyarimana alichaguliwa tena kuwa makamu wa kwanza wa rais anayeshughulikia utawala na masuala ya fedha huku Richard Mugisha akichaguliwa kuwa makamu wa pili wa rais anayeshughulikia maendeleo ya ufundi. 

Munyantwali ambaye amewahu kuhudumu kama meya wa eneo la Nyamagabe alisema anafuraha kuja kutumikia soka nchini Rwanda.  

 "Napenda soka, nimeicheza na kuishabikia katika maisha yangu yote," alisema rais huyo mteule. 

Zoezi la upigaji kura kumchagua rais wa Shirikisho la soka nchini Rwanda
Zoezi la upigaji kura kumchagua rais wa Shirikisho la soka nchini Rwanda © ferwafa

Nafasi zingine zilizojazwa ni pamoja na; Jean Marie Rugambwa (kamishna wa fedha), Quinta Rwakunda (kamishna wa mauzo na ufadhili), Amani Evariste Turatsinze (kamishna anayesimamia uandaaji wa mechi za ligi mbalimbali).

Hamdan Habimana (kamishna wa ufundi na maendeleo ya soka), Ancille Munyankana (kamishna wa soka la wanawake) , Louis Rurangirwa (kamishna wa usalama na maadili katika michezo).

Claudine Gasarabwe (kamishna wa sheria), Herbert Gatsinzi (kamishna wa afya), huku Vedaste Ngendahayo akiwa kamishna anayesimamia timu za taifa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.