Pata taarifa kuu

Atakumbukwa Kwa Kipi Katibu Mkuu wa FIFA Fatma Samoura

Nairobi – Na mchambuzi wetu Paul Nzioki

Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samoura, anayeondoka
Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samoura, anayeondoka © CHRISTOPHE ARCHAMBAULT/AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirikisho la kandanda duniani FIFA chini ya uongozi wake Giann Infantino limedhibitisha kuwa katibu mkuu Fatma Samoura ataacha kazi mwishoni mwa 2023.

Hakuna sababu za msingi zilizotolewa kuhusu hatua hiyo ila inaarifiwa kuwa Samoura amesema anataka kuipa familia yake na majukumu yake mengine muda wa kutosha. Kisa sawa na hiki tumekishuhudia kule Rwanda kiongozi wa Shirikisho la Soka nchini humo Ferwafa Olivier Mugabo Nizeyimana alipoacha kazi kwa madai ya majukumu binafsi kuwa mengi.

Katika taarifa, ya kumuaga FIFA imemtaja kama kiongozi aliyesaidia kurejesha uaminifu wa shirikisho baada ya kashfa ya miaka mingi chini ya Sepp Blatter ambayo ilifikia kilele kupewa #FIFAGate na kukamatwa huko Zurich mwaka 2015.

Chini ya Samoura hatujasikia kesi kubwa ya ufisadi yenye uzito kama ilivyokua kwa Makatibu waliotangulia.

Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samoura ataachana na wadhifa huo mwishoni mwa mwaka huu
Katibu mkuu wa FIFA, Fatma Samoura ataachana na wadhifa huo mwishoni mwa mwaka huu FIFA/AFP

Samoura alivunja rekodi ya kuwa katibu mkuu wa kwanza wa FIFA wa kike na asiyetoka barani Ulaya.

Katibu huyo ameacha alama gani katika soka ?

Tutamhukumu kama waafrika kwa sababu Mwafrika kuwa katika uongozi wa FIFA tulitarajia mengi kama bara.

Katika mkutano huko Paris Ufaransa, Rais Infantino alizungumzia namna uteuzi wa Samoura umesaidia FIFA. Kusema ukweli FIFA imemtumia Samoura kutengeneza picha yao.

Kwa ufupi Samoura alikua skrini kuonyesha Fifa wana uhusiano mzuri na umma . Lakini pia FIFA ilitaka kuwa na mtu kutoka bara lingine ndiyo wafunike ile kauli ya "FIFA ni chama cha bara Ulaya’’.

Fatma Samoura, alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa FIFA kutoka nje ya bara Ulaya
Fatma Samoura, alikuwa katibu mkuu wa kwanza wa FIFA kutoka nje ya bara Ulaya AFP

Ebu tujikumbushe kidogo, Mwaka 2019, Samoura alitumwa kama 'Kamishena Mkuu wa FIFA kwa Afrika' kwenda Cairo kusafisha Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF). Alifanya nini?

Wakati wa utawala wake, mkataba wa upeperushaji mechi wa CAF uliogharimu dola bilioni 1 ukiwa na kampuni ya Ufaransa Lagardère Sports ulighairiwa.

Ni katika utawala wake, FIFA ilipooneka wazi kuingilia kati maswala ya soka Afrika. Mfano Infantino amekuja kufanyia majaribio Super League barani Afrika wakati UEFA ulaya wameikataa.

Katibu mkuu wa Fifa Fatma Samoura kwenye mkutano wa waandishi wa habari  Saint-Pétersbourg, tarehe 16 Juni 2017
Katibu mkuu wa Fifa Fatma Samoura kwenye mkutano wa waandishi wa habari Saint-Pétersbourg, tarehe 16 Juni 2017 AFP/Archives

Kwa mujibu wa katiba ya FIFA, ukisoma kifungu cha  64 na 65 sheria inamruhusu kuendesha shirikisho kila siku lakini muda mwingi hajakuwa akionekana kuwajibikia majukumu yake kikamilifu.

Kuna wengine waliosema alikua anaangazia maswala ya wanawake. Tuseme ukweli pia ata kama aliangaziwa kwenye Maonyesho ya Dubai 2020 katika hafla ya"kusherehekea wanawake kutoka tabaka zote" pamoja na Christine Lagarde.

Chini ya utawala wake, kulikua na kesi ya unyanyasaji dhidi ya Miguel Macedo, kulingana na New York Times, lakini Samoura hakusema chochote.

Wengi wanahisi kuwa hakuafikia viwango kama walivyotarajia
Wengi wanahisi kuwa hakuafikia viwango kama walivyotarajia Reuters

Hadi sasa anaondoka lakini hatuna ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kinadada, Wakati super league kwa wanaume inaanza.

Anaondoka hatujawaona Marefa wanawake wakiwezeshwa vilivyo katika soka la kimataifa.

Labda kwa wanaomtetea wanaweza kusema, usimamizi wa Infantino ulionyesha kwa namna fulani Samoura aliwekwa kando kwenye masuala ya maamuzi. Infantino ana nguvu nyingi.

Rais wa Fifa Gianni Infantino
Rais wa Fifa Gianni Infantino © AP/Martin Meissner

Samoura anapokea karibu dola milioni 2, pamoja na bonasi ya $ 650,000. Kusema ukweli wachache kwenye soka watamkumbuka na labda wengine wanamfahamu akiondoka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.