Pata taarifa kuu

Declan Rice kuondoka West Ham

NAIROBI – Declan Rice ataondoka West Ham msimu huu, mwenyekiti wa klabu hiyo ya Uingereza David Sullivan amethibitisha.

Declan Rice kuondoka West Ham
Declan Rice kuondoka West Ham REUTERS - DAVID W CERNY
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa kati wa Uingereza, amehusishwa na klabu ya Arsenal, Bayern Munich na  Man United msimu huu, alioongoza West Ham kushinda taji lake la taji la Europa Confrence league dhidi ya Fiorentina.

Mwenyekiti huyo ameeleza kwamba wamekubali kumuachiliwa mchezaji huyo kuondoka licha ya kwamba mkataba wake na klabu hiyo bado unaendelea.

Makubaliano haya yamefanyika baada ya kufanyika kwa mazungumzo kati yake na uongozi wa klabu hiyo.

Rice alikiri mapenzi yake kwa klabu ya West Ham kufuatia ushindi wao dhidi ya Fiorentina japokuwa alikiri kwamba hakuwa na uhakika wa iwapo atasalia katika klabu hiyo msimu ujao.

Declan Rice aliisaidia West Ham kushinda taji la  Europa Conference League
Declan Rice aliisaidia West Ham kushinda taji la Europa Conference League AP - Darko Bandic

Kocha wa West Ham David Moyes mwezi uliopita alikiri kuwa kulikuwepo na uwezekano wa Rice kuondoka katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa Sky Sports, West Ham  wanaomba kulipwa £120m ilikuachana na naohodha wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.