Pata taarifa kuu

Ange Postecoglou ndiye kocha mkuu wa  Tottenham

NAIROBI – Tottenham imethibitisha kumteua Ange Postecoglou kama Kocha Mkuu kwa mkataba wa miaka minne.

Postecoglou ndiye kocha mpya wa Tottenham
Postecoglou ndiye kocha mpya wa Tottenham Action Images via Reuters - LEE SMITH
Matangazo ya kibiashara

Postecoglou ameshinda mataji tano ya ndani pamoja na mataji ya ligi tangu kujiunga na Celtic akitokea Yokohama F Marinos ya Japan mwaka wa 2021.

Tottenham walimaliza kwenye nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza, klabu hiyo ikimfuta kazi meneja wake Antonio.

Raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 57 aliteuliwa kuwa meneja wa Tottenham Hotspur siku ya Jumanne, baada ya kushinda mataji matano katika misimu miwili akiwa na Celtic likiwemo la mataji matatu ya ligi ya Scotland mwaka huu.

Akiwa mchezaji Postecoglou alikuwa mlinzi wa South Melbourne katika iliyokuwa ligi ya Soka ya kitaifa kati ya 1984 na 1993, akishinda mataji mawili ya ubingwa, la mwisho kama nahodha.

Alishinda mechi nne kwa Australia kabla ya jeraha la goti kukatisha taaluma  yake ya uchezaji mapema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.