Pata taarifa kuu

Tottenham kumsajili kocha wa Celtic Ange Postecoglou kuwa meneja wake mkuu

NAIROBI – Tottenham inatarajiwa kumsajili meneja wa Celtic Ange Postecoglou kama kocha wao mpya kwa mujibu wa taarifa za watu wa karibu na mazungumzo kati ya klabu hiyo ya Uingereza na kocha huyo.

Ange Postecoglou kocha wa Celtic
Ange Postecoglou kocha wa Celtic AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Postecoglou anadaiwa kukubali kuingia katika mkataba wa miaka mwili na Spurs hatua hii ikija baada yake kuisaidia Celtic kushinda taji katika ligi ya Scotland msimu huu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 alikwepa maswali ya wanahabari kuhusu hatma yake na Celtic baada ya mechi ya mwisho ya msimu Jumamosi iliyopita.

Tottenham wanahitaji mkufunzi baada ya jaribio la kumsajili kocha wa Feyenoord Arne Slot na kocha wa zamani wa Bayern Munich Julian Nagelsmann kukosa kuza matunda.

Celtic na Spurs hawajazungumzia swala hilo wazi japokuwa taarifa za ndani zimedai kuwa Postecoglou alimwambia Dermot Desmond mmoja wa wamiliki wa Celtic kuwa ana mipango ya kujiunga na klabu hiyo ya Uingereza.

Postecoglou ameshinda mataji tano ya ndani pamoja na mataji ya ligi tangu kujiunga na Celtic akitokea Yokohama F Marinos ya Japan mwaka wa 2021.

Tottenham walimaliza kwenye nafasi ya tano katika ligi ya Uingereza, klabu hiyo ikimfuta kazi meneja wake Antonio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.