Pata taarifa kuu

Soka: Karim Benzema anaondoka Real Madrid

Mchezaji bora wa Ufaransa msindi wa Ballon d'Or Karim Benzema ataondoka Real Madrid mwishoni mwa msimu huu, baada ya misimu 14 akiichezea klabu hiyo ya Uhispania, Real Madris imesema katika taarifa yake Jumapili hii, Juni 4.

Karim Benzema alifikisha mabao 236 kwenye ligi ya Uhispania dhidi ya Almería Jumamosi 29 Aprili 2023.
Karim Benzema alifikisha mabao 236 kwenye ligi ya Uhispania dhidi ya Almería Jumamosi 29 Aprili 2023. © AFP / THOMAS COEX
Matangazo ya kibiashara

"Real Madrid CF na nahodha wetu Karim Benzema wameafikiana kumaliza kipindi chake kizuri na kisichoweza kusahaulika kama mchezaji wa klabu yetu," Real Madrid imeandika  katika taarifa iliyotolewa saa chache kabla ya mechi ya mwisho ya msimu wa Ligi Kuu ya Uspania.

Sasa ni rasmi, Karim Benzema ataondoka Real Madrid na kujiunga na ligi ya Saudia.

Miaka 14 ya mafanikio ndani ya Real Madrid

Huu ni mwisho wa historia ndefu ya miaka 14. Karim Benzema alijiunga na klabu ya Real Madrid mwaka wa 2009 kutoka OL kwa euro milioni 35. Mshambuliaji huyo amekuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi katika historia ya Real Madrid kwa misimu hii. Karim Benzema alifanikiwa kujiweka katika nafasi ya kuwa mmoja wa manahodha wa klabu hiyo akiwa na Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos, kisha Marcelo, Luka Modric, Toni Kroos na sasa Vinicius, hadi akawa nahodha. Mshindi wa Ligi ya Mabingwa 5, rekodi kwa mchezaji wa Ufaransa, hata hivyo, alishinda Ballon d'Or mwezi Oktoba mwaka uliyopita. Ni jambo la busara kwa klabu ya Madrid kutangaza kuandaa heshima ya mwisho kwa gwiji wake Jumanne ijayo, Juni 6 katika Jiji la Real Madrid, ambapo atahudhuri hafla hiyo mwenyekiti wa kalbu hiyo Florentino Pérez Rodríguez.

Karim Benzema atajiunga na Al Ittihad ili kuimarisha michuano ya soka nchini Saudia ambapo anacheza mshirika wake wa zamani, CR7, mchezaji wa Al Nassr tangu mwezi Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.