Ombi la Dani Alves wa Brazil kuachiwa kwa dhamana limekatiliwa
NAIROBI – Kesi inayomkabili mlinzi wa timu ya taifa ya Brazil Dani Alves, imeendelea kuwa changamoto kwa upande wake baada ya Jaji wa mahakama mmoja nchini Uhispania kukataa ombi la pili la mchezaji huyo kupewa dhamana.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Haya yamejiri hapo jana siku ya jumanne tarehe 9 mwezi mei 2023 wakati mwanasoka huyo akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake ambayo anakabiliwa na tuhuma za ubakaji.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alizuiliwa mwezi Januari baada ya kushtakiwa kwa kumbaka msichana mdogo katika bafu la klabu ya usiku maarufu night clubs ya Barcelona mwishoni mwa mwaka jana.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Paris Saint-Germain atasalia rumande baada ya mahakama inayomchunguza kusema kuna "hatari kubwa" ya kujaribu kutoroka iwapo ataachiliwa kwa dhamana.
"Mahakama imekataa ombi la kuachiliwa lililotolewa na upande wa utetezi", Mahakama kuu ya haki ya Catalonia ilisema Jumanne utajiri wake "unaweza kumruhusu kuondoka Uhispania wakati wowote".
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa timu ya wanasheria wa Alves kushinikiza kuachiliwa kwake baada ya ombi lao la kwanza kukataliwa mnamo Februari.
Mawakili wake waliomba dhamana tena mwezi Aprili mwaka huu, muda mfupi baada ya kufika mbele ya hakimu kwenye kikao cha pamoja ambapo walisema kuwa wawili hao walikuwa na mahusiano ya kimapenzi lakini wakadai kwamba walikubaliana.
Timu ya mawakili ya Alves ilipendekeza kubatilisha pasi zake mbili za kusafiria, za Brazil na Uhispania, ili kumhakikishia hakimu kwamba anaweza kupewa dhamana wakati huu - lakini ombi hilo lilikataliwa.