Pata taarifa kuu

Tathmini ya Guardiola kuelekea Mechi ya Nusu Fainali klabu bingwa.

NAIROBI – Na Paulo Nzioki

Pep Guardiola, Kocha wa Manchester City
Pep Guardiola, Kocha wa Manchester City AP - Dave Thompson
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya mechi ya Jumanne usiku  ya nusu fainali ya kwanza ya ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Bernabeu, kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola ameipongeza Real Madrid kwa rekodi yao katika mashindano hayo na jinsi ambavyo kikosi cha Madrid kimejiimarisha.

Pep ameulizwa kuhusu nia ya City ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo bado hawajafanya hivyo, kwa miaka mingi.Hata hivyo, alichagua kuangazia umuhimu wa kuendelea kucheza kwa kiwango cha juu, kama ilivyo kwa Real Madrid.

Man city wamefika angalau robo fainali kwa miaka sita iliyopita, lakini wametinga fainali mara moja tu, waliposhindwa na Chelsea mnamo 2021. Los Blancos, wameshinda shindano hilo mara tano katika miaka 10 iliyopita.

"Siku moja tutafika fainali na tutashinda," amesema Guardiola.

Chelsea walishinda kombe la klabu bingwa mwaka wa 2021
Chelsea walishinda kombe la klabu bingwa mwaka wa 2021 Pool via REUTERS - DAVID RAMOS

Guardiola, ni dhahiri shahiri anaifahamu vyema rekodi ya Real Madrid kwenye mashindano haya na anakiri kwamba ili kuwa bora zaidi ni lazima kuwashinda walio bora zaidi.

Katika Ligi ya Mabingwa, Madrid ndio bora na hiyo ndiyo changamoto kwa timu yake katika siku 10 zijazo.

"Ili kushinda shindano hili lazima ushinde timu bora, na Madrid ndio timu bora katika mashindano haya katika muongo uliopita," Guardiola alisema.

Real Madrid ndio ya kwanza kwa vilabu vyenye thamani zaidi duniani
Real Madrid ndio ya kwanza kwa vilabu vyenye thamani zaidi duniani © AFP / ANDER GILLENEA

Ingawa simulizi rahisi katika mtanange huu inaweza kuwa kwamba Guardiola na City wako tayari kulipiza kisasi baada ya kuondolewa na Madrid katika hatua hiyo hiyo mwaka jana, kocha huyo ameyapinga maneno hayo .Kwa Guardiola, sio kulipiza kisasi, ni fursa mpya tu ya kutinga fainali.

"Itakuwa kosa kubwa kutafuta nafasi ya kulipiza kisasi, hatuko hapa kwa ajili ya kulipiza kisasi, ni fursa tu," aliongeza Guardiola.

"Msimu uliopita tulifanya kila kitu, zaidi ya kila kitu kufika fainali, lakini katika soka... haitoshi." alisema kocha huyo wa Mancity

Mchezaji wa Manchester City Haaland na kocha wake Pep  Gardiola
Mchezaji wa Manchester City Haaland na kocha wake Pep Gardiola © goal

Mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali hii ya kusisimua itachezwa mjini Madrid siku ya Jumanne, na marudiano Jumatano ijayo mjini Manchester katika uwanja wa Etihad Guardiola akiwa nyumbani.

Kwa mujibu wa mashabiki wengi na wadadisi wa maswala ya soka la ulaya, atakayeshinda katika nusu fainlai hii ana nafasi kubwa ya kua mshindi wa taji hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.