Pata taarifa kuu

Uchambuzi: Ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa nchini Tanzania

Na: Paul Nzioki

Sehemu ya kuchezea, uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Sehemu ya kuchezea, uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam © tanzanianationalstadium
Matangazo ya kibiashara

Uwanja wa Benjamin Mkapa nchini Tanzania bila shaka ndio uwanja bora kwa sasa katika ukanda wa Afrika Mashariki, ila kuna sehemu ambazo zinahitaji kufanyiwa ukarabati.

Hii ni baada ya miezi kadhaa iliyopita, kamati maalumu ya kukagua maandalizi ya michuano ya CAF Super League, ya Bara Afrika kutua nchini Tanzania, na kufanya kikao cha pamoja na viongozi wa Simba.

Baada ya kamati teule ya kuchunguza sehemu zinazohitaji mabadiliko kufanya vikao, ripoti yao ipo tayari. Moja ya sehemu za kufanyiwa ukarabati ni eneo la kuchezea.

Kamati hiyo imeshauri sehemu ya kuchezea kuwa haipo katika viwango vinavyotakiwa  kwa ajili ya mashindano hayo na inatakiwa kufanyiwa marekibisho makubwa na kubandikwa mchanganyiko wa nyasi asilia na za  kisasa.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinaonesha uwekaji wa nyasi hizo ni wa haraka na unaweza kutumia kati ya siku sita hadi saba.

Hata hivyo, inaonekana ni nyasi bora kabisa kwa maendeleo ya soka kwani zina uwezo mkubwa kulinda afya za wachezaji wanaozitumia, zinawafanya wachezaji kuwa na hali ya kujiamini lakini kukimbia kwa kasi zaidi lakini zikiwafanya wachezaji kuwa na ubora wao kwa muda mrefu.

Pia, kamati hiyo imesema mitambo ya umwagiliaji maji kwenye uwanja huo inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kila sehemu inapata maji ya kutosha. Ukarabati huo unatakiwa kukamilika Agosti 1, 2023.

Sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam © tanzanianationalstadium

Sehemu ya pili ni kwenye magoli na vibenderakwa mujibu wa ripoti ya kamati hiyo,iliyoandikwa na Gazeti la michezo la Mwanaspoti, magoli yaliopo kwenye Uwanja wa Mkapa pamoja na vibendera kwenye eneo la kupigia kona vinatakiwa kubadilishwa.

Siku za hivi karibuni katika mechi mbili za kiwango cha CAF zilizochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam, zimeishia kwa kugonga vichwa vya habari.

Sio kwa Tukio la mechi moja mbali ni katika mechi mbili taa zikipungua mwanga. Katika mechi ya simba dhidi ya Wydad mechi ilisitishwa kwa mda lakini katika mechi ya yanga dhidi ya Rivers United.

Hatua hiyo imekua ni mwendelezo wa maswali mengi ambayo yamekua yakiulizwa kuhusu uwanja bora kwa sasa katika ukanda wa afrika Mashariki.

Pia, Serikali ya Tanzania pia kwa ushirikiano na Shirikisho la mchezo wa soka nchini humo TFF na walifanya kazi ya kukagua miundombinu ambayo itatumika kwenye michuano hiyo.

Marekebisho yote yanatarajiwa kufanyika katika kipindi cha wiki sita hadi nane, kuanzia Mei 15 mwaka huu, huku Kamati ikiamuru kuwa kwa kipindi hicho hawataruhusu mashindano yoyote kufanyika hapo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.