Pata taarifa kuu

Tanzania: Simba yaondolewa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika

NAIROBI – Na Paul Nzioki

Wachezaji wa klabu ya Simba SC nchini Tanzania
Wachezaji wa klabu ya Simba SC nchini Tanzania © SimbaSCTanzania
Matangazo ya kibiashara

Wawakilishi wa ukanda wa Afrika mashariki kutoka nchini Tanzania kwenye ligi ya mabingwa Afrika, Simba SC, wametolewa nje baada ya kushindwa na Wydad Casablanca ya Morocco kupitia mikwaju ya penalti.  

Mechi hio iliishia katika matuta ya penalti baada ya kukamilika kwa jumla ya goli moja kwa moja katika mikondo yote miwili. 

Robo fainali hiyo ilivutia mashabiki takribani mashabiki 45,000 katika uwanja wa Stade Mohammed V. 

Mashabiki wa  Wydad Casablanca katika mechi ya awali.
Mashabiki wa Wydad Casablanca katika mechi ya awali. AFP - -

Raia wa Senegal Bouly Sambou aliipa Wydad goli la kusawazisha katika dakika ya 24 ya mchezo.  

Simba ilikua mbele kwa goli la baleke alilofunga katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. 

Mlinda lango wa Wydad El Motie aliibuka shujaa katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwajumitatu ya penalti kati ya mitano ya Simba iliyopigwa na Shomari Kapombe na raia wa zambia Clatous Chama, huku Wydad wakifunga nne. 

Mashabiki wa Simba ya nchini Tanzania
Mashabiki wa Simba ya nchini Tanzania © simba

Wydad ndio mabingwa watetezi achia mbali kushinda taji hili la klabu bingwa barani Afrika mara tatu. 

Ushindi kwa Wydad unamaanisha ni mechi yao ya saba ya nusu fainali tangu 2016 katika mashindano ya kwanza ya vilabu barani Afrika ambayo ni rekodi. 

Watamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini au Cr Belouizdad ya Algeria katika nusu fainali mwezi Mei. 

Wachezaji wa  Mamelodi Sundowns.
Wachezaji wa Mamelodi Sundowns. © Courtesy of CAF

Sundowns wanaongoza kwa mabao 4-1 na wanaikaribisha Belouizdad katika mechi ya mkondo wa pili wa robo fainali utakaochezwa Jumamosi. 

Kuondolewa kwa Simba katika michuano hii, ina maana kwamba bado wataendelea kusaka mafanikio ya kufuzu kuelekea hatua ya nusu fainali katika mashindano ya CAF. 

Katika misimu miwili iliyopita Wekundu wa msimbazi wamecheza katika kombe la klabu bingwa na Kombe la shirikisho wakitolewa katika hatua ya Robo fainali. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.