Pata taarifa kuu

FIFA yapokea zabuni nne za kuandaa kombe la dunia la wanawake 2027

NAIROBI – Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA limepokea zabauni nne za Mataifa yanayotaka kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake mnamo 2027. 

 Gianni Infantino, Rais wa FIFA
Gianni Infantino, Rais wa FIFA FIFA/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Afrika kusini ndio taifa pekee kutoka barani Afrika lililojitokeza kutoa zabuni yao wakiwa na nia ya kutaka kuwa wenyeji wa mashindano hayo.

Mataifa mengine ambayo yamewasilisha zabuni zao ni Brazil wakati Ubelgiji, Uholanzi na Ujerumani yakizindua onyesho la pamoja. 

Marekani na Mexico pia zimewasilisha zabuni yao ya pamoja kuandaa michuano hiyo. Siku ya mwisho ya kuwasilisha zabauni kwa FIFA ni tarehe 19 mwezi Mei mwaka huu.  

Waandaji wanatarajiwa kuchaguliwa na Shirikisho la Fifa kupitia upigaji kura wa hadhara tarehe 17 Mei 2024. 

katibu mkuu wa Fifa Fatma Samoura amesema shirikisho hilo limefurahi kupokea zabuni hizo hatua inayoonyesha nia ya mataifa hayo kuandaa mashindano hayo. 

Mabingwa watetezi wa kombe hilo Marekani waliandaa michuano hiyo mwaka wa 1999 na 2003, huku Ujerumani wakiwa wenyeji wa michuano hiyo mwaka wa 2011. 

Kombe la Dunia la 2023 litafanyika Australia na New Zealand kati ya 20 Julai na 20 Agosti. 

Marekani, Mexico na Canada watashiriki Kombe la dunia la wanaume mwaka wa 2026. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.