Simba kuwasilisha malalamishi dhidi ya mashabiki wa Wydad kwa CAF
NAIROBI – Klabu ya Simba ya nchini Tanzania, inawazia kuwasilisha kesi dhidi ya tabia za mashabiki wa klabu ya Wydad Athletic Club wakati huu wakijandaa kupambana katika mechi ya nduru ya pili katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hatua ya Simba inakuja baada ya ushindi wao wa goli moja bila ya jibu dhidi ya Wydad ambao ndio mabingwa watetezi wa ligi ya Mabingwa CAF.
Kabla ya kuondoka nchini tanzania kuelekea Morocco, Simba itawasilisha rasmi malalamishi yao kwa Shirikisho la Soka barani Afrika CAF kufuatia matukio ambayo mashabiki wa Wydad waliyoyafanya kwenye uwanja wa Mkapa katika kipindi cha dakika10 za mwisho kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Mashabiki wa Wydad Athletic Club wanatuhumiwa kwa kuingia katika eneo la jukwaa moja la watu mashuhuri la VIP B bila ya kupewa kibali.
Kwa mujibu wa taarifa iliochapishwa na gazeti za Mwanaspoti nchini Tanzania, Mashabiki hao wamekuwa wakiambatana na timu hiyo kila mahali wanapokwenda na wanatajwa kuwa na vurugu kubwa kwenye mechi za ugenini kuliko nyumbani kwao.
Baada ya kuruka uzio huo wakati wa mechi hiyo, waliwasha fataki za moshi ambao uliwazuia mashabiki wengine kuona pamoja na wachezaji na waamuzi kuona giza hali iliyomfanya mwamuzi kusimamisha mchezo.
Msimu uliopita Simba iliwahi kukabiliwa na kasheshe la mashabiki kama hao wakipambana na RS Berkane ya Morocco.
Baada ya simba kuripoti wakati huo CAF iliwapa adhabu Berkane kwa kuwapunguzia idadi ya mashabiki kwenye mechi zao.
Baadhi ya video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii ni sehemu ya ushahidi ambao maafisa wa klabu ya simba wamekusanya kama njia moja ya kujenga hoja katika kesi yao.
Sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa timu za kaskazini kuwasha vitochi katika uwanja hasa wakati timu zao zinakua hazifanyi vyema uwanjani.