Chelsea wanakaribia kumteua Mauricio Pochettino kama Kocha Mkuu
NAIROBI – Chelsea wanakaribia kumteua aliyekua kocha wa zamani wa Paris Saint Germain Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mkuu.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Pochettino ndiye kocha anayepewa nafasi kubwa zaidi ya kupewa ya kuchukua nafasi ya kocha mkuu na inaripotiwa kuwa kuna ongezeko la mazungumzo ya ambayo huenda yakafanikiwa.
Meneja huyo wa zamani wa Tottenham, ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka Paris Saint-Germain msimu uliopita, amepewa nafasi hiyo kubwa haswa baada ya Julian Nagelsmann kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho mwishoni mwa juma lililopita.
Pochettino amefanya mfululizo wa mazungumzo na wamiliki wa Chelsea na inafahamika kwamba uthibitisho wa raia huyo wa Argentina kuwa mrithi wa kudumu wa Graham Potter unaweza kuja hivi karibuni.
Imesisitizwa, hata hivyo, kwamba mpango huo haujakamilika na kwamba klabu hiyo inawazia kuhusu wagombea wengine iwapo mazungumzo kati yake na Pochettino yatavunjika.
Wamiliki wenza wa Chelsea, Todd Boehly na Behdad Eghbali, wako chini ya shinikizo la kufanya uteuzi sahihi baada ya timu kuendelea kupata matokeo yasiyo mazuri chini ya mkufunzi wa muda Frank Lampard ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Chelsea.
Chelsea ilimpa Frank Lampard majukumu ya muda baada ya kumfuta kazi Potter mwezi huu.
Pochettino, ambaye uhusiano wake na Spurs hauwezekani kuwa kizuizi kwa kuchukua kazi hiyo, atakuwa meneja wa tatu wa kudumu kufanya kazi chini ya umiliki huu mpya iwapo atapewa kazi hiyo.
Potter, ambaye alikuwa kwenye wadhifa huo kwa miezi saba pekee, aliletwa baada ya kutimuliwa kwa Mjerumani Thomas Tuchel Septemba iliyopita ambaye kwa sasa ndiye kocha wa Bayern Munich.