Pata taarifa kuu

Mastaa wa Soka barani Afrika waliofilisika baada ya ndoa zao Kuvunjika

NAIROBI – Na Mchambuzi wetu Paulo Nzioki

Soka ni sehemu ya ajira
Soka ni sehemu ya ajira © Getty Images/iStock/Artisteer
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wengi wa mpira wa miguu  ambao ni maarufu huwa katika hatari ya kukumbwa na matatizo mengi katika maisha.  Baadhi ya changamoto zao ni ndoa zao kuvunjika na matokeo yanawaathiri hadi wanafilisika.

Baadhi ya wachezaji kutoka Afrika waliojipata katika changamoto hiyo:

Taribo West 

Staa huyu raia wa Nigeria alifilisika baada ya talaka na kwa sasa ameamua kuwa mchungaji kabisa. 

Taribo ambaye alioana na Minigeria mwenzake Atinuke Ekundayo kisha baadaye mwana mama huyo alielekea mahakamani kudai talaka. 

Baada ya hakimu kupitisha kesi ya Atinuke, West aliyewahi kuzichezea Inter Milan na AC Milan kati ya mwaka 1997 hadi 2000, alimlipa fidia na ndugu akashuka viwango sana kifedha.  

Asamoah Gyan 

Mashabiki wengi wa soka wanamfahamu gwiji huyu raia wa raia na penalti aliyoipoteza katika robo fainali ya michuano ya Kombe la dunia mwaka 2010 Afrika kusini. 

Lakini pia matatizo ya wanandoa yaliwahi kumfika. Mwezi Oktoba mwaka 2018, ripoti kutoka vyombo vya Afrika na Ulaya zilieleza mchezaji wa zamani wa Ghana, Asamoah Gyan amefilisika baada ya kuachana na mkewe Gifty Gyan. 

Asamoah Gyan Mchezaji wa zamani wa Ghana
Asamoah Gyan Mchezaji wa zamani wa Ghana ASSOCIATED PRESS - Luca Bruno

Gyan baadaye alidhibitisha kuwa amebaki na Pauni 600 tu kwenye akaunti yake ya benki. 

Hata hivyo, aligutuka kabla ya hali kuwa mbaya zaidi na mali yake yote akaiandika chini ya jina la kakake ikiwemo nyumba, magari na mali nyingine. 

Kisa cha kuvunja mbavu katika kesi ya Gifty na Gyan ni kuwa naye Gyan aliomba watoto wafanyiwe vipimo vya DNA ili kubaini kama ni wake au asilipe fidia. 

Emmanuel Eboue 

Hakuna binadamu anayeishi chini ya jua anayetamani yaliyomfika raia huyu wa Ivory Coast na Staa zamani wa Arsenal kumfika siku hata moja. 

Ni mmoja kati ya wachezaji ambao wameacha funzo kubwa kwa wachezaji wa Kiafrika. 

Aliachana na mke wake wa kwanza Aurelie aliyekua naye bila mali kisha alipopata sabuni ya roho akamtafuta kichuna aliyekwenda skuli kasoma sheria.

Emmanuel Eboué akiwa mchezaji wa Arsenal
Emmanuel Eboué akiwa mchezaji wa Arsenal Reuters

Eboue anasimulia pesa zote za usajili na mshahara alizokuwa anazipata alikuwa akimpa mkewe na kuna muda alikuwa anasaini makaratasi bila kujua kama alikuwa ni makubaliano ya kumrithisha mkewe mali zake. 

Kama ilivyo kwa wachezaji wengi wa kiafrika, kufahamu lugha za kigeni ni tabu na ndio iliokua sababu kubwa ya Eboue kusaini asichokifahamu. 

Emmanuel Eboue mchezaji wa zamani wa Ivory Coast
Emmanuel Eboue mchezaji wa zamani wa Ivory Coast AP - THOMAS KIENZLE

Baadae kidosho alidai Talaka, Eboue akapoteza kila kitu na kurudi kwao Ivory Coast kuanza upya. 

Hata hivyo, baada ya mahojiano yake, timu mbalimbali ikiwemo Arsenal na Galatasaray zilijitokeza na kumpa nafasi ya kufanya nao kazi kwa sasa yupo zake Ivory Coast ambako amefungua akademia ya kulea wachezaji ambao baada ya muda hupelekwa barani Ulaya. 

Gumzo mtaani hivi karibuni kimekua ni kisa cha raia wa Morocco anayeichezea PSG, Achraf Hakim na namna ambavyo Mamake alifanya harakati za kumuokoa mwanaye kwa kumiliki asilimia kubwa ya mshahara wake. 

PSG Achraf Hakimi wa PSG na Morocco
PSG Achraf Hakimi wa PSG na Morocco DeFodi Images via Getty Images - DeFodi Images

Hakim ambaye alifunga ndoa na mkewe, Hiba Abouk mwaka 2020, kesi yake labda imetoa funzo kwa wachezaji wengi. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.