Pata taarifa kuu

Rwanda: Rais wa FERWAFA Olivier Nizeyimana ajiuzulu

NAIROBI – Rais wa Shirikisho la Soka la Rwanda, FERWAFA, Olivier Nizeyimana, amejiuzulu kutoka kwa wadhifa wake.

Aliyekuwa rais wa FERWAFA nchini Rwanda
Aliyekuwa rais wa FERWAFA nchini Rwanda © RBA
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake Jumatano mchana, Mugabo amesema amejiuzulu kwa sababu za kibinafsi ikiwa ni pamoja na kile alichokiita "kazi nyingi." 

Katika barua iliyoandikwa kwa wanachama wote wanaounda bodi ya kandanda ya nchi hiyo, Nizeyimana alisema "Nimeona kwamba kuchanganya [kazi ya Shirikisho] na majukumu mengine itakuwa na athari mbaya." 

"Ninashukuru sana kwa juhudi zenu kwa malengo yetu tuliyokamilisha pamoja na msaada wenu mzuri katika maendeleo ya soka nchini Rwanda," aliongeza. 

Nizeyimana alichaguliwa, bila kupingwa kama rais wa FERWAFA mnamo Juni 28, 2021. 

Wakati huo, alichukua nafasi ya Brig. Jenerali Jean-Damascène Sekamana ambaye alijiuzulu Aprili mwaka huo. 

Niyezimana anamiliki kampuni ya usafiri, Volcano Express, na pia anaendesha biashara ya ndani ya Hyundai. 

Kiongozi huyu amejiuzulu wakati huu nafasi ya timu ya taifa Amavumbi ikiwa finyu sana katika michuano ya kufuzu kuelekea Kombe la Mataifa ya Bara Afrika. 

Rwanda wapo katika kundi na moja na Benin, Misri na Msumbiji ambapo wana alama tatu baada ya kucheza mechi nne. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.