Pata taarifa kuu

Mambo Manne Ya Kuangalia Wikendi Hii Katika Ligi Kuu Ya Uingereza

NAIROBI – Na Mchambuzi wetu Paul Nzioki

 Bukayo Saka,Mchezaji wa Arsenal
Bukayo Saka,Mchezaji wa Arsenal REUTERS - DAVID KLEIN
Matangazo ya kibiashara

Ligi kuu nchini England maarufu kama EPL itaendelea wiki hii ikiwa ni raundi ya thelathini. Katika Makala haya tunaangazia mambo manne muhimu ya kuangalia kama shabiki wa Ligi hii wikendi hii. 

Arsenal watapata ushindi Anfield? 

Msimu uliopita Arsenal walipata kichao cha magoli 4-0 katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool Anfield. 

Arsenal, hawajashinda Liverpool kwa zaidi ya miaka 10 wakiruhusu mabao 37, wakiambulia vipigo viwili vya 5-1, viwili vya 4-0 pamoja na vichapo vitatu 3-1 wakati huo. 

Wachezaji wa klabu ya Arsenal
Wachezaji wa klabu ya Arsenal © AFP - GLYN KIRK

Kwa sasa kiwango cha Liverpool kinadidimia na huu ndio wakati mwafaka wa Kocha Mikel Arteta kumshinda mwenzake Jürgen Klopp. 

Liverpool dhidi ya Arsenal, Jumapili saa 10 Jioni

Mwendelezo wa Ten Hag 

Zimesalia mechi 10 za Ligi ya premia kwa Manchester United kushinda pointi za kutosha ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.  

Tayari kocha mkuu Erik Ten Hag amesema hili linawezekana na ni lazima. 

Nafasi ya nne sio nafasi ambayo labda iliwafaa United lakini itakua muhimu kwa mabingwa hawa mara 20. 

Ziara ya Everton ni mechi ya mwisho ambayo Casemiro atalazimika kukaa nje kwa sababu ya kufungiwa mechi nne na, huku Christian Eriksen akiwa kwenye mzozo tena baada ya kukosekana kwa sababu ya jeraha tangu Januari. 

Erik Ten Hag meneja wa Manchester United
Erik Ten Hag meneja wa Manchester United IKIMAGES/AFP/File

Siku ya Jumatano, kuifunga Brentford kulipandisha kikosi cha Ten Hag hadi pointi 53, tatu mbele ya Tottenham katika nafasi ya tano wakiwa na mchezo mkononi, hivyo wanadhibiti hatima yao. 

Chelsea na Kocha Mpya 

Ni chini ya Kocha Mpya Frank Lampard aliyepewa nafasi hii hadi mwisho mwa msimu huu ambapo anakua meneja wa tatu wa msimu huu. 

Kama ataufuata muundo wa Chelsea ya sasa inayoonekana kama timu ya kawaida basi mabao yatakuwa magumu kufikiwa. 

Chelsea ya sasa ina Kai Havertz juu, ambaye alikuwepo katika sare ya bila kufungana na Liverpool katikati ya wiki.  

Frank Lampard, aliyekuwa meneja wa muda wa Chelsea
Frank Lampard, aliyekuwa meneja wa muda wa Chelsea Reuters

Wachache sasa wanaamini Havertz atakuwa mchezaji hodari katika rangi ya bluu kama alivyokua Diego Costa. 

Wolves dhidi Chelsea, Jumamosi Saa Tisa mchana

Southampton Wanahitaji kuwasaidia Arsenal 

Southampton wanajua mengi kuhusu Manchester City. Waliajiri mkuu wao wa kuajiri, kutoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu msimu uliopita.  

Joe Shields ameendelea kuleta vijana kutoka akademia ya City.  

Gavin Bazunu na Romeo Lavia wameonyesha ubora wa Ligi Kuu, wakati Samuel Edozie na Juan Larios wakifurahia dakika chache uwanjani siku za hivi karibuni. 

Wachezaji wa Liverpool na Chelsea katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza.
Wachezaji wa Liverpool na Chelsea katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza. AP - Frank Augstein

Wikendi hii Mancity anakaribishwa uwanjani St. Mary's ambapo akiteleza na ashindwe kupata alama tatu, kisha Arsenal ashinde mechi yake na Liverpool safari ya Ubingwa msimu huu itasalia kua Hadithi. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.