Pata taarifa kuu

Carlo Ancelotti anawataka Benzema, Modric na Kroos kusalia Real Madrid

NAIROBI – Carlo Ancelotti anaamini kuwa Karim Benzema, Luka Modric na Toni Kroos watasalia katika klabu ya Real Madrid msimu ujao.

Kocha wa Real Madrid anawataka Benzema, Modric na Kroos kusalia katika klabu hiyo
Kocha wa Real Madrid anawataka Benzema, Modric na Kroos kusalia katika klabu hiyo REUTERS - ISABEL INFANTES
Matangazo ya kibiashara

Watatu hao wanamaliza mkataba mwishoni mwa msimu huu na Ancelotti alithibitisha Modric na Kroos sasa wanazungumza na klabu hiyo kuhusu mustakabali wao.

Benzema alijiunga na Real Madrid kutoka Lyon mwaka wa 2009 na Modric aliwasili kutoka Tottenham mwaka 2012, wawili hao wameshinda Ligi ya Mabingwa mara tano na Real Madrid kati ya mataji mengine.

Toni Kroos alijiunga na Madrid akitokea Bayern Munich mwaka 2014, na kushinda klabu bingwa barani Ulaya mara nne akiwa na Los Blancos.

Alipoulizwa kuhusu Kroos na Modric, Ancelotti alisema anaamini "suluhisho" litapatikana.

"Kuna maendeleo, kwa sababu wanazungumza, nadhani mwishowe watatafuta suluhu, kuna maendeleo." amesema Ancelotii.

 Kocha huyo pia alidhani Benzema, ambaye alifunga hat-trick katika ushindi mnono wa 4-0 dhidi ya Barcelona Jumatano kwenye nusu fainali ya Copa del Rey, angesalia.

Ancelotti bado anaamini kwamba Benzema, Modric na Kroos wanaipa Madrid mengi, hata kama wamevuka kilele chao.

“Lazima tuwatathmini wachezaji si kwa umri wao bali kwa kile wanachofanya,” aliongeza kocha huyo.
 "Unaweza kudhani watatu hawana wasifu au nguvu ya wachezaji wachanga, lakini walichonacho watatu hawa katika usimamizi wa mchezo ni wa kipekee, huwezi kununua kwenye soko lolote duniani, Hii inazaliwa na uzoefu ,umri huchukua kitu kutoka kwako, lakini hukupa kitu pia."alisisitiza kocha huyo.

Madrid itamenyana na Villarreal kwenye La Liga Jumamosi, kabla ya kuwakaribisha Chelsea Jumatano kwenye mechi ya mkondo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.