Pata taarifa kuu

Haaland kukosa mechi mbili zijazo za Norway kufuzu Euro 2024

NAIROBI – Shirikisho la soka nchini Norway limesema mshambuliaji wa timu ya taifa  Erling Haaland atakosa mechi mbili zijazo za kufuzu kuwania taji la bara Ulaya dhidi ya Uhispania na Georgia kutokana na jeraha la paja.

Erling Haaland kukosa mechi mbili za Norway kufuzu Euro 2024
Erling Haaland kukosa mechi mbili za Norway kufuzu Euro 2024 AFP
Matangazo ya kibiashara

Haaland, ambaye hivi majuzi alifunga mabao matano kwa klabu yake ya Manchester City dhidi ya Leipzig kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga mabao matatu dhidi ya Burnley kwenye Kombe la FA, alipopata jeraha hilo.

Aidha uongozi wa soka nchini humo umesema Haaland ameondoka kwenye kambi ya mazoezi ya timu ya taifa huko Marbella, Uhispania,  kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na klabu yake ya Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester City. 

Norway itacheza mechi mbili za ugenini katika mechi ya kwanza ya kundi A ya kufuzu kwa Euro 2024, ya kwanza dhidi ya Uhispania huko Malaga Jumamosi na Georgia huko Batumi Jumanne. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.