Pata taarifa kuu

Mechi za robo fainali kuwania klabu bingwa barani Ulaya

NAIROBI – Mabingwa watetezi Real Madrid watacheza na Chelsea katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa huku Manchester City wakipangwa dhidi ya Bayern Munich katika droo iliyofanyika siku ya Ijuma.

Fainali ya klabu bingwa barani Ulaya itachezwa mjini Istanbul Jumamosi, Juni 10.
Fainali ya klabu bingwa barani Ulaya itachezwa mjini Istanbul Jumamosi, Juni 10. © REUTERS/Murad Sezer
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa Serie A Napoli watachuana na AC Milan katika mchuano utakaozikutanisha timu zote kutoka Italia wakati Inter Milan wakipangwa dhidi ya  na vinara wa ligi ya Ureno Benfica.

Washindi wa mechi ya Real dhidi ya Chelsea watakutana na City au Bayern katika nusu-fainali.

Mechi za kwanza za robo-fainali zitachezwa Aprili 11 na 12, huku Real wakiwakaribisha Chelsea kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu kwanza kabla ya kusafiri London kwa marudiano wiki moja baadaye, na City wakiwa nyumbani kwa Bayern kwanza.

Inter walipangwa kucheza na Benfica nyumbani awali lakini sasa watasafiri hadi Lisbon kwa mechi ya kwanza ili kuepusha pambano kati ya AC Milan na Napoli huko San Siro.

Nusu fainali itachezwa mwezi Mei wakati  fainali ikipangwa kupigwa  mjini Istanbul ikipangwa Jumamosi, Juni 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.