Pata taarifa kuu

Messi ndiye Mchezaji bora wa FIFA mwaka wa 2022

NAIROBI – Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Paris St-Germain Lionel Messi, ndio mchezaji bora Shirikisho la soka duniani FIFA, kwa mwaka 2022. 

Virgil van Dijk, Lionel Messi, Kylian Mbappe baada ya kutuzwa kama wachezaji bora wa FIFA 2022
Virgil van Dijk, Lionel Messi, Kylian Mbappe baada ya kutuzwa kama wachezaji bora wa FIFA 2022 AP - Michel Euler
Matangazo ya kibiashara

Messi mwenye umri wa miaka 35 aliwashinda wachezaji wa timu ya taifa ya  Ufaransa Kylian Mbappe na Karim Benzema kunyakua taji hilo. 

Raia huyo wa Argentina alikuwa nahodha wa timu hiyo wakati  alipoisaidia kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Qatar mwaka uliopita. 

Katika msimu wa mwaka wa 2021 na 2022, Messi alifunga mabao 27 katika michezo 49 za klabu na nchi yake kati ya mwaka wa 2021 na 2022.  

Kwa upande wa wanawake, Alexia Putellas wa Barcelona ndio mshindi. 

Lionel Scaloni ambaye aliiongoza Argentina kushinda taji lao la tatu la Kombe la Dunia, alichaguliwa kama kocha bora wa mwaka wa wanaume.  

Scaloni aliwashinda Pep Guardiola aliyeisaidia Manchester City kushinda taji la sita la Ligi kuu ya Uingereza na kocha wa Real Madrid aliyeshinda Ligi ya Mabingwa na klabu hiyo, Carlo Ancelotti.  

Mlinda mlango wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 30 alishinda tuzo la mlinda mlango bora upande wa wanaume,naye Muingereza Mary Earps akishinda tuzo ya wanawake.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.