Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA KENYA

Kenya: Afc Leopards na Gor Mahia wanakutana Kwenye Debi la Mashemeji

Mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia wanakutana na wapinzani wao wa jadi AFC Leopards mabingwa mara 12, katika mchezo wao wa 93 katika Debi la Mashemeji, Jumapili kwenye Uwanja wa kitaifa wa Nyayo, Nairobi. 

WACHEZAJI WA AFC LEOPARDS YA KENYA
WACHEZAJI WA AFC LEOPARDS YA KENYA © AFC LEOPARDS
Matangazo ya kibiashara

Ni debi la zamani zaidi katika historia ya soka ya Kenya. Mechi kali ambayo kila shabiki wa soka nchini kenya anaisubiri. 

Timu zote mbili zinanolewa na Makocha wa kigeni, Mskoti Jonathan Mckinstry wa Gor Mahia na Mwenzake Mbelgiji Patrick Aussems wa AFC Leopards. 

Pande zote mbili zilikutana kwa mara ya kwanza Mei 5 1968 na wamekuwa wapinzani tangu wakati huo huku Gor Mahia wakifurahia rekodi nzuri ya ushindi mara 7 katika mikutano yao ya hivi majuzi. 

Jambo la kuhuzunisha zaidi ni kwamba Leopards bado haijasajili ushindi dhidi ya Gor Mahia tangu Machi 6, 2016 wakati Mshambuliaji Lamine Diallo aliwapa pointi zao tatu za mwisho kwenye debi. Ni rekodi ambayo Ausemms atakuwa na nia ya kuivunja. 

Kufikia sasa Gor wako katika nafasi ya tatu kwenye jedwali wakiwa na pointi 23, pointi sita mbele ya Leopards walio katika nafasi ya saba huku timu zote zikisajili ushindi katika mechi zao tatu za mwisho kwenye ligi. 

K'ogalo wanajivunia kiwango kizuri cha Mshambualiji wao chipukizi Benson Ochieng Omalla ambaye amefanikiwa kupachika wavuni mabao 10 katika mechi 10.   

Ingwe ikitegemea huduma za raia wa Nigeria Kingsley Olaniyi Fasanmi ambaye amaefunga magoli 5 kwa usaidizi mkubwa wa winga stadi Cliff Nyakeya ambaye amekuwa akitamba pembeni mwake. 

Na Paul Nzioki

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.