Pata taarifa kuu
SOKA-UCHAMBUZI

Changamoto za uhamisho kwa wachezaji wa soka Afrika Mashariki

Na: Mchambuzi wetu, Paul Nzioki

Uwanja wa  Nelson Mandela nchini Algeria
Uwanja wa Nelson Mandela nchini Algeria AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa soka katika nchi za Afrika Mashariki, wanaendelea kupitia changamoto mbalimbali ambazo zisipopewa suluhu ya haraka, zitarudisha nyuma mafanikio hayo.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja uhamisho ni mazingira magumu ya kucheza soka, mivutano katika familia miongoni mwa mengine mengi.

Leo tuangazie changamoto ya uhamisho wa wachezaji: Swali la usajili tata wa kiungo wa Yanga, Feisal Salum  limemalizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka (TFF).

Bila ya kukaa na viongozi kujadili uamuzi na sababu zake za kuondoka, Salum  aliamua kuvunja mkataba wake na Yanga ambao umesalia mwaka mmoja zaidi kwa kulipa Sh100 milioni na mshahara wa miezi mitatu wa Sh12 milioni.

Kamati hiyo iliamua mchezaji huyo wa kimataifa bado ni mali ya mabingwa hao wa soka Tanzania ligi kuu Bara. Swala la Fei Toto kama wanavyomuimba watanzania limenitia mshawasha wa kuandika Makala haya.

Kanuni za soka zinatoa utaratibu wa kutosha kwa wachezaji na wanaohusika na biashara ya kuuza na kununua wachezaji. Huwezi kuamka tu kama mchezaji wa soka na ukaamua kuondoka.

Wachezaji wengi Afrika Mashariki wana taabu wanapoachana na vilabu vyao. Kwa mfano, sakata la Feisal lilikua la mshtuko mkubwa kwa kua klabu haikuwahi kuwa na matatizo naye ya kimasilahi wala kiufundi.

Sababu Za Wachezaji Kuhama:

Maslahi: Kuna wachezaji wengi ambao wamelalamika kuhusu mishahara wanayopokea, magari wanayoendesha na nyumba wanazoishi. Ni moja ya sababu ambazo uenda zikamtia motisha mchezaji kuhama. Suala hili linatakiwa liendelee kuwa la muajiri na muajiriwa tu.

Mazingira: Sio mara moja au mbili tumesikia mchezaji akisema hakupenda mazingira ya klabu yake ya awali. Hili linaweza kutokana na Mashabiki, Mabosi au Wachezaji wenzake. Kwa mfano wachezaji wengi waliocheza Afrika kusini wametoa lawama kama hizi.

Mafanikio Kimataji: Mashabiki wengi wa mpira wanaamini kama unacheza barani ulaya na unataka kufanikiwa kwa ngazi ya klabu bingwa ulaya, sharti ucheze katika timu ya Real Madrid.

Vivyo hivyo kama utautaka ubingwa wa Afrika ucheze Al Ahly, Wydad Casablanca au Mamelodi sundowns. Miaka mitano nyuma Tp Mazembe wangekuwa mojawapo ya timu hizi. Kwa hivyo mchezaji anaweza kuondoka iwapo atahisi anachokitaka ni kikubwa kuliko lengo la timu yake.

Suluhu ni nini

Kuna ngazi mbili za mazungumzo katika suala la uhamisho. Moja ni kua mchezaji anamilikiwa na timu. Pili mchezaji ana wakala wake. Ofa rasmi lazima ifikie klabu ndio timu iwasiliane na wakala wa mchezaji kwa kuzingatia mkataba.

Suala la tatu ni makubaliano binafsi ambapo anausishwa mchezaji aidha kupitia wakala wake au meneja. Kwa hivyo, Lazima kuwepo kwa makubaliano ya pande zote mbili ,waajiri na waajiriwa.

Kama mwanasoka hufai kuondoka klabuni kwa njia ambayo itakushtaki mbele ya macho ya watu kama mhuni. Mchezaji pia ukijua unaihama klabu yako sio vyema uwe unatuma video kila mara mitandaoni kuonesha huko uendako ni bora kuliko uliko sasa.

Katika historia ya mpira waliondoka kwa purukushani katika vilabu vyao kuna heshima waliyoikosa. Kaisome historia au unitafute kijiweni nikuadithie maisha ya Claude Makelele, aliyewahi kuwa mchezaji mkubwa Real Madrid ya Hispania.

Kuna sababu kwanini leo hii bado Ronaldo de Lima anaheshimika Real Madrid, Barcelona, AC Milan na Inter Milan. Messi ameondoka Barcelona lakini bado wanacatalunya wanamheshimu.

Eden Hazard aliondoka Chelsea lakini bado yupo kwenye nyoyo zao. Samatta aliondoka TP Mazembe lakini bado wanampenda. Boniface Ambani aliondoka Yanga lakini bado wanampenda ata baada ya kustaafu.

Kwa wachezaji ambao wanataka kuvihama vilabu vyao. Nawashauri kuwa mda sahihi wa kuihama klabu yako ni wakati wa dirisha kubwa.  Makocha wengi niliowahi kupiga stori na wao walinieleza kua dirisha dogo ni la kuziba mianya tu. Achana na wanaokaribia kustaafu, ni nyota wachache sana huhama Januari.

Mameneja na mawakala wetu barani Afrika sijui uelewa wao wa mpira kama taasisi umefika wapi. Ajabu kubwa ni kua wachezaji wetu wanafanya makosa makubwa sana wakiwa mikononi mwa Mameneja.

Sasa natoa changamoto kwa mameneja na mawakala, kwamba wapeni wachezaji elimu ya kutosha kuhusu mikataba na maisha ya mpira. Kama mawakala pia lazima mjue kutetea masilahi ya Mteja wako wakati wa kujadili mkataba. Inatakiwa na uangalie si tu kiwango cha mshahara wakati huo lakini na pia wakati mwingine ukifika mtake kuufanya uhamisho itakuaje.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.