Pata taarifa kuu
Oleksandr Usyk-Deontay Wilder-Pigano

Mapigano yalioratibiwa kufanyika mwaka huu wa 2023

Mwaka huu wa 2023 kumeratibiwa kupigwa mapambano kadhaa katika ulimwengu wa ndondi ambapo:

Tyson Fury .
Tyson Fury . REUTERS - STEVE MARCUS
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa wapinzani Anthony Joshua na Deontay Wilder, Tommy Fury, Jake Paul,Chris Eubank Jr na Conor Benn watakutana, itakuwa ni mojawapo ya mpambano wa kusisimua.

Kwingineko washindani wa zamani Ricky Hatton na Manny Pacquiao nao wanatarajiwa ulingoni, Mashabiki wa Pacquiao wakiwa na kiu cha kumuona akipigana tena.

Ila zaidi ya yote Pambano kubwa ambalo mashabiki wa ndondi wanataka likamilike ni pambano la uzani wa juu kati ya Tyson Fury na Oleksandr Usyk wa Ukraine.

Baada ya kutangaza kustaafu baada ya kumpiga Dillian Whyte mnamo Aprili mwaka wa 2021 mfalme wa Gypsy alirudi kazini mnamo Desemba.

Bingwa huyo wa uzito wa juu wa WBC aliwaita Usyk na Anthony Joshua kabla ya kumalizana na Derek Chisora.

Fury alivutia wakati wa mzunguko wa 10 na alitazamwa na WBA (Super), IBF, WBO na mshikilizi wa taji la dunia la IBO Usyk.

Baadaye Fury na Usyk walikutana ana kwa ana na wamepangwa kupigana mapema mwaka huu.

Hakujawa na bingwa asiyepigwa katika uzani wa juu tangu mkanda wa WBO uanze kutambuliwa kama taji kuu na enzi ya mikanda minne kuanza.

Fury amedai kuwa pambano la muungano dhidi ya Usyk, ambaye alimpiga Anthony Joshua mapema mwaka huu, litakua 'rahisi' kuliko lile dhidi ya Chisora.

 

Na Paul Nzioki

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.