Pata taarifa kuu
SENEGAL-MANE-QATAR

Jeraha lamweka nje Sadio Mane, mechi za kombe la dunia

Mchezaji bora wa soka barani Afrika, Sadio Mane, haitoichezea timu yake ya taifa ya Senegal kwenye michuano ya kombe la dunia, inayoanza siku ya Jumapili nchini Qatar baada ya daktari wake, kusema jeraha alililolipata halitakuwa limepona.

Mshambuliajie wa Senegal Sadio Mane, aliyepata jeraha
Mshambuliajie wa Senegal Sadio Mane, aliyepata jeraha © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya Daktari wa Senegal Manuel Afonso, iliyotumwa kwa njia ya video katika ukurasa wa Twitter wa Senegal, imewavunja moyo mashabiki wa Senegal, baada ya awali mchezaji huyo kujumuishwa katika kikosi cha mwisho kwa matumaini kuwa atakuwa amepona.

“Inasikitika kuwa uchunguzi wa MRI unaonesha kuwa, hali yake haijaimarika, hatuna lingine ila kumwondoa katika kikosi kitakachoshiriki kwenye kombe la duni,” alisema Daktari Afonso.

Mane alikuwa anaichezea klabu yake ya Bayern Munich mapema mwezi huu, wakati alipopata jeraha.

Mechi ya kwanza ya Senegal itakuwa dhidi ya Uholanzi, Jumatatu ijayo.

Imepangwa katika kundi la A na wenyeji Qatar, Ecuador na Uholanzi.

Kikosi cha wachezaji 26, kilichotajwa:

Makipa

  • Edouard Mendy (Chelsea)
  • Alfred Gomis (Rennes)
  • Seny Dieng (QPR)

Mabeki

  • Kalidou Koulibaly (Chelsea)
  • Pape Abou Cisse (Olympiacos)
  • Fode Ballo-Toure (AC Milan)
  • Ismail Jakobs (Monaco)
  • Formose Mendy (Amiens) 
  • Abdou Diallo (RB Leipzig)
  • Youssouf Sabaly (Real Betis)

Viungo wa Kati

  • Idrissa Gueye (Everton)
  • Pathe Ciss (Rayo Vallecano) 
  • Cheikhou Kouyate (Nottingham Forest)
  • Pape Gueye (Marseille)
  • Krepin Diatta (Monaco) 
  • Nampalys Mendy (Leicester City) 
  • Pape Matar Sarr (Tottenham)
  • Mamadou Loum (Reading)
  • Moustapha Name (Pafos)

Washambuliaji

  • Sadio Mane (Bayern Munich)
  •  Boulaye Dia (Salernitana)
  •  Bamba Dieng (Marseille)
  •  Ismaila Sarr (Watford)
  • Iliman Ndiaye (Sheffield United)
  • Famara Diedhiou (Alanyaspor)
  •  Nicolas Jackson (Villarreal)
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.