Sadio Mane kukosa mechi ya kwanza ya kombe la dunia dhidi ya Uholanzi
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Senegal, Sadio Mane, atakosa mechi ya kwanza ya kombe la dunia, dhidi ya Uholanzi, Jumatatu ijayo nchini Qatar, kufuatia mchezaji huo kuendelea kuuguza jeraha.
Imechapishwa:
Mane mwenye umri wa miaka 30, alitajwa kwenye kikosi cha wachezaji 26 kushiriki kwenye fainali ya kombe la dunia, licha ya kuwa na jeraha la mguu, alilopata wakati, akiichezea klabu yake ya Bayern Munich.
Kocha Aliou Cisse amesema, mshambuliaji huyo hahitaji upasuaji, na ana imani kuwa atapona haraka na kucheza mechi ya pili.
“Tutacheza mechi ya kwanza bila Sadio na tutashinda bila ya uwepo wake,” amesema Abdoulaye Sow kiongozi wa soka nchini Senegal.
Raia wa Senegali wanaomwombea mchezaji wao apone haraka, wakiongozwa na rais Macky Sall.
Ratiba ya michuano ya kombe la dunia:
Jumapili, Novemba 20, 2022: Qatar vs Ecuador
Jumatatu, Novemba 21, 2022: Uingereza vs Iran
Senegal vs Uholanzi
Marekani vs Wales
Jumanne, Novemba 22, 2022:Argentina vs Saudi Arabia
Denmark vs Tunisia
Mexico vs Poland
Ufaransa vs Australia
Jumatano, Novemba 23, 2022: Morocco vs Croatia
Ujerumani vs Japan
Hispania vs Costa Rica
Ubelgiji vs Canada