Pata taarifa kuu

Mpira wa kikapu: FIBA yachunguza tukio la mchezaji wa Mali kumpiga makonde Mserbia bada ya mechi

Shirikisho la mchezo wa kikapu duniani, FIBA, linachunguza tukio la wachezaji wawili wa timu ya taifa ya wanawake ya Mali kupigana baada ya mechi yao ya kombe la dunia, dhidi ya Serbia hapo jana. 

Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Mali Touty Gandega, hapa wakati wa mechi dhidi ya Japan, Septemba 22, 2022 huko Sydney, Australia.
Mchezaji wa mpira wa kikapu wa Mali Touty Gandega, hapa wakati wa mechi dhidi ya Japan, Septemba 22, 2022 huko Sydney, Australia. AP - Mark Baker
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji wa Mali, Salimatou Kourouma alionekana kwenye mkanda wa vídeo akimpiga makonde matatu mchezaji mwenzake, baada ya mechi yao kumalizika kwa kufungwa kwa vikapu 81 kwa 68. 

Mali ambayo haijashinda mechi yoyote mpaka sasa, inacheza mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi hivi leo dhidi ya Canada, katika mashindano hayo yanayoendelea jijni Sydney, Australia. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.