Pata taarifa kuu
LIGI KUU-SOKA

Klabu za soka nchini Kenya, zaapa kutoshiriki mechi za ligi kuu

Na: Paul Nzioki

Mpira wa miguu
Mpira wa miguu AFP
Matangazo ya kibiashara

Vilabu vya ligi kuu kandanda nchini kenya, vimetoa tamko la kutoshiriki katika msimu mpya wa ligi kuu nchini, utakaoandaliwa na kamati ya mpito au shirikisho la soka kabla ya kuhidhinishwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Raymond Oruo, afisa mkuu mtendaji wa Klabu ya Gor Mahia aliyesoma ujumbe wa vilabu kwa niaba ya timu 18 za ligi kuu , amesema kwamba wao kama vilabu hawatogharamika kucheza ligi ambayo haitambuliwi na FIFA.

‘’Tumekubaliana kama vilabu vya ligi kuu kandanda nchini kenya,kwamba timu zetu hazitoshiriki katika ligi yoyote ile kabla ya marufuku tuliyopewa na FIFA kuondolewa . Vilabu vyetu msimu uliopita vilishiriki katika ligi ambayo haikutambuliwa na FIFA, wenzetu Tusker walishinda ligi na hawachezi katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika, hii ni hasara kubwa’’ amesema Raymond.

"Ilikua ngumu hata kufanikisha uhamisho wa wachezaji na kwa ajili ya mchezo wetu kitaifa, ni ligi tu iliyoidhinishwa na shirikisho la soka duniani itakayotupeleka mbele."

Wito huo wa vilabu vya KPL unajiri siku moja tu baada ya Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Nick Mwendwa kutangaza kwamba msimu mpya utaanza baada ya mwezi mmoja.

Mwendwa aliahidi kuiandikia Fifa ili adhabu ya kufungiwa iliyowekewa nchi Februari 24 na shirikisho hilo iondolewe.

Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks, Mathare United, City Stars, Sofapaka, Tusker, Bidco United ni miongoni mwa klabu 13 zilizotuma wawakilishi wao.

Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari, afisa mkuu mtendaji wa timu ya Nairobi city stars, Patrick Korir, amekiri kua hawajakutana na Mwendwa kupanga njia ya kuendeleza suala hilo. Aidha Korir amesisitiza kwamba wanataka kucheza tu kwenye ligi inayotambulika na Fifa bila kujali nani anaongoza.

"Yeyote anayetaka kuendesha ligi ambayo Fifa haitambui anapaswa kujua kwamba hatutashiriki," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Nairobi City Stars Patrick Korir.

Hata hivyo wawakilishi hao wa vilabu, wamekataa kujibu swala la kupanda au kushuka kwa gazi katika ligi kuu.

Mwakilishi wa Nairobi city stars akisema kwamba wanazungumza kwa niaba ya vilabu vilivyoshiriki ligi kuu msimu uliopita na wala hawahusiani na maswala ya kupandisha timu kucheza ligi kuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.