Pata taarifa kuu
KENYA-LIGI KUU

Soka nchini Kenya: Msimu mpya wa ligi kuu kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti

Na: Paul Nzioki

Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya Gor Mahia.
Mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Kenya Gor Mahia. Yasuyoshi CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msimu mpya wa Ligi kuu nchini kenya unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu  wakati huu ambapo vilabu vinakumbwa na changamoto za fedha.

Msimamizi wa shughuli za vilabu katika kamati ya Mpito inayosimamia soka nchini kenya, Ali Amour, ameeleza kuwa wamo katika mazungumzo na serikali kama njia moja ya kutatatua sintofahamu iliyoko.

“Fedha ni changamoto kubwa lakini tunaendelea kuomba serikali itusaidie ndio tuvisaidie vilabu, ila nao wenye vilabu nchini kenya wanafaa kujua mpira ni biashara,” anaeleza Bwana Amour.

Hatua hii inakuja wakati huu ambapo baadhi ya vilabu vikitishia kuwa huenda havitashiriki ligi hiyo kwa misingi kuwa haitambuliwi na Shirikisho la michezo duniani FIFA.

Ali Amour ambaye ni mfanyibiashara na mshika dau katika soka kwa mda mrefu nchini kenya, amelijibu swala hilo kwa swali, “Mimi nina swali kwao, kwa sababu kama ligi haitambuliwi na FIFA, ni kwa nini vilabu vyetu kama AFC Leopards na Gor mahia wamepewa adhabu ya kutosajili ? ”.

Ali ameongeza kuwa, baadhi ya wenyekiti kama vile mwenyekiti wa Klabu ya Mathare Bob Munro, ni sheria hawataki kufuata kwa kusema kwamba hawahifahamu kamati hio kisheria, baada ya kuwashusha daraja.

Changamoto za waamuzi katika Ligi Akizungumzia swala la waamuzi amesema kuwa wamepokea madai ya maamuzi mabovu ya waamuzi na wapo tayari kutoa mafunzo na kuzichunguza rekodi za waamuzi kabla ya kuwateua kusimamia mechi.

Bwana Ali akifanya mahojiano na Mwanahabari wetu wa michezo Paul Nzioki, amekiri kuwa tatizo la maamuzi mabovu wamelipata katika mpira wa kenya bado likiangaziwa ila halijaanza wakati wao.

Masharti ya vilabu kufuata kabla Msimu Mpya kuanza. Kabla Ligi kuanza lazima kila timu iwasilishe data zao kama vile mikataba yao na wachezaji, kwa kamati, jambo ambalo tayari wameafikiana na baadhi ya vilabu.

Kamati hiyo aidha imesisitiza kuwa ipo tayari kuendeleza shughuli za michezo nchini kenya hadi pale mda wao wa kuwa afisini utaisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.