Pata taarifa kuu
Kenya - Michezo

Kenya: Serikali yafuta mashtaka dhidi ya Nick Mwendwa

Afisi ya kiongozi wa mashtaka nchini Kenya (DPP) imefuta mashtaka ya rushwa dhidi ya aliyekuwa mwenyekiti wa shirikisho la mchezo wa soka nchini humo, FKF, Nick Mwendwa kwa mjibu wa kifungu cha 87  cha adabu cha katiba ya taifa hilo.

Alyekuwa aais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa
Alyekuwa aais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Nick Mwendwa twitter.com/nmwendwa
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inatokana na afisi ya DPP kukosa mashahidi katika kesi hiyo, na ombi la kutaka jDPP, kutaka muda zaidi ili kutafuta mashahidi limekataliwa na  jaji Eunice Nyuttu ambaye amemuachilia huru  bwana Mwendwa.

Jaji huyo pia amelaumu afisi ya DPP kwa kuwakatawa shukukiwa na kuwafikisha mahakamani bila kuwa na ushahidi wa kutosha.

Serikali ya Kenya, mwaka uliopita mwezi Novemba, ilivunja kamati yote ya shirikisho la FKF, waziri wa michezo Amina Muhamed akiteua kamati ya muda kuendesha shughuli soka nchini Kenya.

Kutokana na hatua hiyo shirikisho la soka duniani FIFA, lilipiga marufuku Kenya, kutokana na muingilio wa serikali ndani ya FKF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.