Pata taarifa kuu
AWCON 2022

Michuano ya soka kutafuta taji la wanawake yaendelea kushika kasi

Michuano ya soka kuwania taji la soka barani Afrika kwa upande wa wanawake, inaendelea wiki hii jijini Rabat nchini Morocco.

Timu ya taifa ya Nigeria, Super Falcon ikishiriki kwenye michuano iliyopita
Timu ya taifa ya Nigeria, Super Falcon ikishiriki kwenye michuano iliyopita Premium Times Nigeria
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu, kuna michuano ya kundi C ambako Nigeria itachuana na Afrika Kusini, huku Burundi nayo ikicheza na Botswana.

Matokeo ya kundi A:

Morocco 1-0 Burkina Faso

Senegal 2-0 Uganda

Kundi B:

Cameroon 0-0 Zambia

Tunisia 4-1 Togo

Ratiba ya Julai 4, 2022

Kundi C

Nigeria vs Afrika Kusini

Burundi vs Botswana

Wakati uo huo, Shirikisho la soka barani Afrika limetangaza kuongeza kiwango cha fedha anazôpata mshindi wa mashindano haya kwa asililia 150, kutoka Dola za Marekani kutoka 975, 000 hadi 2, 400 ,000

Mshindi wa kwanza atapokea  Dola 500, 000, mshindi wa pili Dola 300, 000 na mshindi wa tatu Dola 200, 000. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.