Pata taarifa kuu
WAFCON 2022

Uchambuzi: Nani ana nafasi ya kushinda taji la soka la wanawake barani Afrika?

Nairobi – Wiki iliyopita, Shirikisho la soka barani Afrika CAF, lilitangaza droo ya hatua ya makundi kuelekea mashindano ya mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake. Michuano hiyo itafanyika nchini Morocco, mwezi Julai.

Timu ya taifa ya Nigeria-Super Falcons
Timu ya taifa ya Nigeria-Super Falcons Premium Times Nigeria
Matangazo ya kibiashara

Kwa timu zote kumi na mbili, nne zitashiriki kwa mara ya kwanza tangu mashindano haya kuasisiwa mwaka 1991.

Ni mataifa mawili tu (Nigeria na Equatorial Guinea) ndio yamewahi kushinda ubingwa wa bara Afrika.

Kundi A: Morocco, Burkina Faso, Senegal na Uganda

Morocco ambao ni waandalizi wanashikiri kwa mara tatu pamoja na Senegal na Uganda ambao itakua mara yao ya pili kila mmoja. Burkina Faso wamefuzu kwa mara ya kwanza. Uganda walifuzu kwa faida ya Kenya kukosa kushiriki raundi ya mwisho ya muondoano baada ya kuifunga Sudan jumla ya mabao 15-1. Ni miaka 22 tangu Uganda iliposhiriki mara ya kwanza na ya mwisho.

Kundi B: Cameroon, Zambia, Tunisia naTogo

Cameroon walioandaa mashindano ya wanaume mwaka huu ni miongoni mwa washiriki mara nyingi zaidi (12) sawa na Nigeria, Ghana na Afrika Kusini (11). Cameroon vile vile wamefanikiwa kufika hatua ya fainali mara nne bila kufanikiwa kushinda taji. Tunisia na Zambia wanashiriki kwa mara ya pili na tatu mtawalia ilhali Togo ni mara ya kwanza.

Kundi C: Nigeria, Afrika Kusini, Burundi na  Botswana

Hili ndilo kundi la mibabe, kundi la kufa kupona, linalojumuisha mabingwa mara nyingi wa kombe hili, Nigeria (11) na Afrika Kusini ambao wamefanikiwa kufika kwenye fainali mara tano ikiwemo makala yaliyopita 2018 nchini Ghana. Kisha Botswana na Burundi wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Timu zinapokutana mara nyingi, kila mmoja hua na uwezo wa kuusoma mchezo wa mpinzani. Hivyo basi, Afrika Kusini na Nigeria zinafahamiana vizuri kuliko Botswana na Burundi ambao hakuna yeyote anayefahamu mchezo wao. Ila tajriba ya muda mrefu huchangia pakubwa kuandikisha matokeo ya kuridhisha kwenye mashindano.

Mashindano haya yatakamilika tarehe 23 mwezi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.