Pata taarifa kuu

AFCON 2021: Je, itakuwa Cameroon au Misri kucheza na Senegali fainali ?

Wenyeji Cameroon wanaingia dimbani Alhamisi usiku, kuchuana na Misri katika mechi ya pili ya nusu fainali, kuwania kombe la mataifa ya Afrika.

Mshambuliaji wa Cameroon Karl Toko Ekambi
Mshambuliaji wa Cameroon Karl Toko Ekambi © Pierre René-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

Mechi hii itakayochezwa kwenye uwanja wa Olembe jijini Yaoundé, inawakutanisha miamba wa soka barani Afrika na ni kama fainali ya mwaka 2017 iliyochezwa nchini Gabon. Cameroon ilishinda Misri mabao 2-1 na kuibuka mabingwa.

Misri ambao wameshinda taji hili mara saba, huku Cameroon wakinyakua mara tano.

Mbali na kuwa nyumbani, Cameroon inawategemea washambuliaji Vincent Aboubakar ambaye mpaka sasa anaongoza kwa ufungaji wa mabao, hadi hatua ya robo fainali, alikuwa ametikisa nyavu mara sita.

Hata hivyo, mshambuliaji mwingine Karl Toko-Ekambi anayecheza soka nchini Ufaransa katika klabu ya Olympic Lyonnais, naye ni wa kutazwa sana.

Hadi sasa Ekambi, ameifungia timu yake mabao matano. Mechi ya robo fainali dhidi ya Gambia, iliyomalizika kwa Cameroon kupata ushindi wa 2-0, alifunga mabao yote.

Mo Salah anayesaka taji la AFCON kwa nchi yake ya Misri
Mo Salah anayesaka taji la AFCON kwa nchi yake ya Misri REUTERS/Amr Abdallah Dalsh

Misri nayo inamtegemea mshambuliaji wake Moahmmed Salah, anayechezea klabu ya Liverpool nchini Uingereza, kuiongoza Pharaoh katika hatua ya fainali, kumenyana na Senegal iliyoishinda Burkina Faso mabao 2-1 katika ya nusu fainali ya kwanza, Jumatano usiku. Fainali itachezwa siku ya Jumapili.

Kuelekea katika mechi hii, kocha Misri Carlos Queiroz amemshtumu rais wa Shirikisho la soka la Cameroon na mchezaji wa zamani Samwel Eto'o kwa kuwaambia wachezaji wa Cameroon kuwa mechi yao ya nusu fainali ni vita.

Kupitia ujumbe wa video, Eto'o aliwaambia wachezaji wa nchi yake wajiandae vema kwa sababu wanakwenda vitani.

Kocha Queiroz amesema ujumbe huo ni wa vitisho na sio mzuri kuelekea katika mchezo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.