Pata taarifa kuu
CAF SUPER CUF-AL AHLY-SOKA

Al Ahly yanyakua ubingwa wa CAF Super Cup

Klabu ya Al Ahly ya Misri ndio mabingwa wa taji la CAF Super Cup, baada ya kuishinda Raja Casablanca ya Morocco kwa penalti 6-5 baada ya timu zote kutoka sare ya bao moja kwa moja, katika fainali iliyochezwa nchini Qatar Jumatano usiku.

Wachezaji wa  'Al Ahly, baada ya kuishinda Raja Casablanca kuwania taji la CAF Super Cup, Desemba 22 2021 nchini Qatar
Wachezaji wa 'Al Ahly, baada ya kuishinda Raja Casablanca kuwania taji la CAF Super Cup, Desemba 22 2021 nchini Qatar AFP - KARIM JAAFAR
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa Al Ahly Taher Mohamed na  Akram Tawfik walifanya kazi ya ziada kuisaidia klabu yao kupata ushindi huo, muhimu baada ya Mohamed kusawazisha bao moja walililokuwa wamefungwa katika dakika tisini ya mchezo huo.

Raja Casablanca walionekana kuelekea kupata ushindi, baada ya kuanza kufunga katika dakika ya 13 ya mechi hiyo baada ya mkwaju wa Abdelilah Madkour kumchanganya beki wa Al Ahly Yassir Ibrahim aliyeugusa mpira na kuingia nyavuni.

Hili ni taji la nane la Al Ahly, klabu inayofunzwa na kocha kutoka Afrika Kusini Pitso Mosimane.

 

Historia ya washindi wa taji la CAF Super Cup

-Al Ahly imeshinda mara nane- 2002, 2006, 2007, 2009, 2013, 2014, 2021 , 2021

-Zamalek mara nne- 1994, 1997, 2003, 2020

-TP Mazembe mara tatu- 2010, 2011, 2016

-Etoile du Sahel mara mbili-1998, 2008

-Raja Casablanca mara mbili- 2000, 2019

-Enyimba mara mbili- 2004, 2005

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.