Pata taarifa kuu
SOKA-MICHEZO

Soka: Liverpool na Salah waawadhalilisha Manchester United na Ronaldo

Liverpool imepata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Manchester United  kwenye uwanja wake Jumapili hii 24 Oktoba 2021 katika mchezo mkubwa wa ligi kuu ya nchini Uingereza.

Mmisri Mohamed Salah, aliyefunga mabao matatu ya Liverpool kwenye uwanja wa Manchester United, Oktoba 24, 2021, katika mechi ya Ligi  kuu ya Uingereza.
Mmisri Mohamed Salah, aliyefunga mabao matatu ya Liverpool kwenye uwanja wa Manchester United, Oktoba 24, 2021, katika mechi ya Ligi kuu ya Uingereza. REUTERS - PHIL NOBLE
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Salah, mchezaji kutoka Misri, ameingiza mabao matatu kwa niaba ya Liverpool. Winga huyo wa Liverpool aliendelea kuwa mfungaji bora wa Afrika katika historia ya Ligi Kuu akiwa na mabao 107, mbele ya Didier Drogba (104) kutoka Côte d'Ivoire.

Manchester United na Liverpool wapinzani wa kihistoria

Mechi ya mwisho iliyowakutanisha vinara hawa wawili, ilikuwa ni mwezi Mei katika dimba la Old Trafford, ambapo hata hivyo mchezo wao ulisogezwa mbele baada ya mashabiki wa United kufanya maandamano kupinga familia ya Glazers inayomiliki klabu hiyo.

Katika mechi hiyo Liverpool waliibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Katika msimamo, United walikuwa wanashikilia nafasi ya 6 kabla ya mechi ya hivi leo ikiwa imeshinda mechi 4 peke yake, ikitoka sare mara mbili na kupoteza michezo mitatu sasa katika mechi tisa ambazo imecheza.

Liverpool kwa upande wao walikuwa kabla ya mechi katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja hadi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.